AMISSI TAMBWE AKANUSHA KUIHAMA SIMBA

Na Regina Mkonde.

Straika wa timu ya wekundu wa msimbazi Simba Amissi Tambwe amekanusha taarifa ambazo zilikuwa zinavumishwa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba amefanya mazungumzo na baadhi ya timu hapa nchini ili ahame Simba.

Maneno hayo aliyazungumza Amissi Tambwe akiwa katika kiwanja cha mazoezi cha Kinesi wakijiandaa na mechi  ya watani wao wa jadi Yanga ambayo itachezwa jumamosi ijayo.

'Mimi sijawahi kuongea na vyombo vya habari juu ya suala hili na hata uongozi wa timu yoyote ile ila ninacho shangaa kusikia kwenye vyombo vya habari kwamba Tambwe anataka kuhama Simba', Alisema na kuongeza straika huyo.


'Mpaka sasa sijapata taarifa yoyote kutoka kwa viongozi wangu ya mimi kuhama isitoshe mkataba wangu bado haujaisha nimesajiliwa Simba mwaka jana mkataba wa miaka miwili inamaana mkataba wangu unaisha mwaka 2015 iweje leo vyombo vya habari vinanivumisha nataka kuhama Simba Sc?', alishangaa mchezaji huyo anayetokea nchi ya Burundi Amissi Tambwe.

'Kuhusu taratibu zetu za kisoka mtu ambaye mkataba wake haujaisha haruhusiwi kusaini mkataba wa timu nyingine labda viongozi wenyewe waamue kuniuza hapo sitakataa ila ninaamini viongozi wangu na wadau wa timu ya Simba Sc hawawezi wakaniuza kwa sasa',aliongeza Tambwe.

Tambwe mpaka sasa ameshikilia rekodi ya mfungaji bora katika msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara inayodhaminiwa na Vodacom Tambwe amefunga magoli 19,  alieleza changamoto alizokutana nazo katika msimu huu na kudai kuwa alisaini mkataba wa Simba ili ahakikishe timu yake inachukua ubingwa lakini hicho kitendo kimekuwa kinyume na kuacha mchezaji huyo abaki njia panda.

Nilijitahidi kweli kufunga katika msimu huu ila ndiyo hivyo timu yangu haijafanikiwa kupata nafasi ya kuchukua ubingwa ingawa baadhi ya watu wanamlaumu kocha Zdravoc Logarusic na kudai kuwa si kocha mzuri mimi siafikiani nao sababu ni kocha anayefaa kupormoka kwa timu ni bahati mbaya tu.Alisema Amis Tambwe.

Tambwe ambaye hapo awali alishawahi kucheza timu kama MountozFc  Black Eagle na Vitalo Fc za nchini kwao Burundi alikuwa akisifika kwa uwezo wake akiwa mpirani na timu zote alizopita Tambwe alikuwa akiongoza kwa kufunga mabao.

Siku chache zilizopita Tambwe alipigwa faini na shirikisho la mpira wa miguu TFF kwa kosa la kutukana akiwa uwanjani tukio hilo lilitokea wakati Simba Sc ilipocheza na Mbeya City Amissi Tambwe baada ya kufunga goli alinyoosha kidole cha shahada ila TFF ilimnukuu vibaya na kumwambia alionyesha kidole cha kati ambacho kinamaanisha tusi.

Tambwe alisikitishwa na kitendo hicho sababu alilipishwa faini ya sh laki tano za kitanzania na kosa hili si sahihi sababu hakuna uthibitisho wa video ulionyesha mchezaji huyo akionyesha ishara ya kunyoosha kidole cha kati ambacho kinatafsiri ni matusi.

Mpaka sasa Tambwe amebakisha mkataba wa mwaka mmoja naye amesema kuwa mechi waliyoibakiza ni ya ushindani mkubwa sababu Simba itacheza na watani wao wa jadi.mechi hii inatakiwa tufunge ili kuleta heshima ya timu ila sitaongea mengi kwa kuwa mchezo hautabiliki ila tunachotakiwa ni kushinda', Alisema Tambwe.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA