DROGBA APOTEZA MATUMAINI YA KUENDELEA NA SOKA USONI

Didier Drogba

Nahodha wa Ivory Coast Didier Drogba ambaye atacheza Kombe la Dunia bado anatafakari kuhusu mustakabali wake katika klabu ya Uturuki ya Galatasaray aliyojiunga nayo Januari 2013 baada ya kipindi kifupi Uchina.
Straika huyo wa miaka 35 alitia saini mkataba wa miezi 18 ambao utaisha Juni, kukiwa hakuna makubaliano ya kuongeza mkataba huo kwa sasa.

Fowadi huyo wa zamani wa Chelsea alisema Alhamisi kwamba anahitaji muda kuchagua kati ya familia yake ambao kwa sasa inaishi Uingereza na soka Uturuki.

“Napenda sana soka ya Uturuki na zaidi klabu yangu ya sasa ya Galatasaray,” Drogba alisema. “Napenda pia familia yangu ambayo inaishi Uingereza, na nafikiri nitalazimika kuchagua kati ya maeneo hayo mawili.
“Nitahitaji muda zaidi kutafakari na kuamua nitakalofanya.”

Drogba amepuuzilia mbali ripoti kwamba yuko karibu kutia saini mikataba na klabu zinazocheza MLS ya Marekani na Serie A ya Italia.


Ataongoza Ndovu kwenye Kombe la Dunia Brazil, Juni ambapo timu yake itakutana na Colombia, Ugiriki na Japan katika ngazi ya Makundi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA