ANELKA KUTOCHEZA BRAZIL

Nicholas Anelka

Klabu cha Brazil Atletico Mineiro kimetangaza wamefutilia mbali mipango ya kumsaini straika wa Ufaransa, Nicolas Anelka.

Mkurugenzi wa timu hiyo Eduardo Maluf amesema kuwa Mineiro wameshindwa katika juhudi zao za kuwasiliana na mshambuliaji huyo aliyechezea Arsenal, Real Madrid, Paris Saint Germain na Chelsea na wamekata tama ya kusajili nyota huyo aliye na umri wa 35.

“Hakuna wakati tulifanikiwa kuzungumza naye,” vyombo vya habari vya Brazil vilinukuu Maluf akisema.

Miniero walidhibitishia AFP kuwa Anelka hatajiunga na gwiji wa Brazil, Ronaldinho, anayesakata kabumbu yake kwenye timu hiyo huku Maluf akiongeza watatuma malalamishi kwa shirkisho la soka duniani, FIFA, kuhusu straika huyo.


Mkurugenzi huyo anashikilia kuwa waliaafikiana na waakilishi wa Anelka lakini wakala wake, Cristian Cazini, aliwapasha habari kuwa mchezaji huyo hatawasili Brazil Jumamosi iliyopita kama ilivyopangiwa.
“Tuliamua kandarasi hiyo imebatilishwa kwani hatutasubiri hadi tarehe 19,” Maluf alifafanua.

Mwenyekiti wa Mineiro Alexandre Kalil alisema Aprili 5 kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuwa Anelka atasaini huku wanahabari wa Brazil wakichapisha picha za mashabiki wa klabu hicho wakibeba mabango ya kumkaribisha straika huyo.

Anelka alisafiri Kuwait kuhudhuria kongamano la vijana wa dini ya Kiislamu badala ya kutua Brazil kukamilisha maagano kati yake na Miniero.

Maluf alifichua kuwa mkataba ulikuwa mezani ukingoja sahihi yake uliaafikia angelicheza nao hadi Desemba mwaka ujao.

Klabu cha Ligi ya Premier ya Uingereza, West Bromwich Albion kilimfuta Anelka mwezi uliopita kwa upotuvu wa nidhamu baada ya kuonekana kuonyesha ishara ya kupinga usemiti ‘quenelle’ baada ya kuwafungia bao.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA