RAIS WA BRAZIL AMUUNGA MKONO DAN ALVES
Swala a tata la ubaguzi wa rangi katika michezo limeibua mchango wa rais wa Brazil.
Rais Dilma Rousseff, amesifu kitendo cha
mchezaji wa kimataifa wa Brazil, na Barcelona Dani Alves kutokana na
tukio la ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya ligi kuu ya Uhispania, La
Liga kati ya Barcelona na Villareal .Bi Rousseff aliandika katika mtandao wake wa twitter kuwa Dani Alves alionyesha ujasiri wa kukabiliana na ubaguzi wa rangi katika kandanda na kuwa ni tukio la kuigwa .
Mamia ya watu na wachezaji maarufu duniani wameonyesha upendo wao kwa mchezaji huyo kwa kuweka picha zao kwenye mitandao wa kijamii wakila ndizi.
Mchezaji wa Manchester City Sergio Aguero alipachika picha akila ndizi sawa na nyota ya soka ya wanawake Marta .
Wengine ni Luiz Suarez wa Liverpool,Oscar, David Luiz na Willian wote wa Chelsea .
Rais wa Fifa sepp Blatter ameongezea sauti yake katika tukio la hivi punde akisema ni vibaya kwa dhulma hizo kuendelea katika karne hii.