Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2026

YANGA PRINCESS SIO WAPINZANI WA SIMBA QUEENS

Picha
Na Prince Hoza Matua  IMEFIKA wakati tuongee ukweli ti ni sio kuficha ficha ni kwamba upinzani wa Simba na Yanga ubaki kwa timu ya wanaume hasa zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania bara, lakini huku kwingine upinzani umeamuliwe na matokeo. Hiyo yote imetokekana na matokeo ya mechi yao ya jana ya Ngao ya Jamii iliyochezwa katika uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam, katika mchezo huo Simba Queens iliondoka na ushindi wa mabao 3-0. Achana na ushindani wao kwenye upande wa wanaume ambao unajulikana kwani kuna wakati Simba inamnyanyasa Yanga na pia Yanga inamnyanyasa Simba. Ukienda kwenye takwimu zao timu gani insongoza kumfunga mwenzake mara nyingi utaons kila moja imewahi kumfunga mwingine, vipigo vikubwa kama vile kumfunga mwenzake mabao 6, 5, 4 ama 3 zote imewahi kufanya hivyo ingawa Simba ndio iliyowahi kumfunga Yanga mabao 6-0. Lakini Yanga imewahi kuwafunga  Simba mabao 5 zaidi ya mara moja, ushindani wa Simba na Yanga au Yanga na Simba umekuwa na upinzani wa kweli kwa maana kila m...

Mayele aonesha pasipoti zake tatu

Picha
Nyota wa DR Congo na mshambuliaji wa Al Ahli Tripoli ya Libya, Fiston Mayele, ameonyesha pasipoti zake mbalimbali alizonazo hivi sasa: Pasipoti ya kawaida ya DR Congo Pasipoti ya utumishi (Service Passport) Pasipoti ya kidiplomasia, baada ya kutunukiwa cheo cha Knight (Fundi/Askari wa Heshima) Mshambuliaji huyo wa DR Congo, ambaye aliiwakilisha nchi yake katika Kombe la Dunia, sasa amerejea Libya kuendelea na msimu akiwa na pasipoti mpya ya kidiplomasia.

Chivayo aliliwa kila kona

Picha
Rais William Ruto wa Kenya ameomboleza kifo cha Rafiki yake Mfanyabiashara wa Zimbabwe Wicknell Chivayo pamoja na Mkewe, vilivyotokea baada ya kupata ajali ya helikopta Nchini Zimbabwe saa kadhaa zilizopita. Katika ukurasa wake wa X, Rais Ruto ameandika “Nimehuzunishwa sana na kifo cha ghafla na cha kusikitisha cha Rafiki yangu Wicknell Chivayo pamoja na Mkewe Lucy Muteke na Watu wengine waliopoteza maisha katika ajali ya helikopta nchini Zimbabwe, kuondoka kwao ghafla ni pigo kubwa kwa familia zao, Marafiki na wote waliowafahamu” “Wicknell alikuwa Rafiki yangu mpendwa ambaye ukarimu na upendo wake uliwagusa Watu wengi, nitamkumbuka kwa urafiki wake, nguvu na ari yake, pamoja na imani yake kubwa katika fursa na uwezo wa Bara letu” “Natoa pole zangu za dhati kwa familia za wote waliopoteza maisha, kwa Rais Mnangagwa, Wananchi wa Zimbabwe na wote wanaoomboleza msiba huu mkubwa, Mungu awajalie Wicknell, Lucy na wote waliofariki pumziko la milele” ameandika Rais Ruto katika ukuraasa wake w...

Kamungo apata pasipoti ya Tanzania

Picha
Mchezaji Mtanzania Bernard Kamungo ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya Congo DR hatimaye amepata hati ya kusafiria ya Tanzania na sasa ataanza kuitumikia Taifa Stars. Kamungo alishindwa kucheza kwenye mchezo kati ya Tanzania na Guinea Bissau pale Amaan Zanzibar kwakuwa hakuwa na passport, mchezo ambao Stars ilichapwa 2-0 nyumbani.