Manqoba: Matokeo hayakuniondosha Yanga ila

KOCHA Manqoba Mngqithi, amedai kuvunjwa kwa mkataba wake na mabingwa hao wa soka Tanzania huenda hakukutokana na matokeo mabaya pekee, akihisi huenda kulikuwa na hujuma zilizochangia kuondoka kwake klabuni hapo.

Kauli ya raia huyo wa Afrika Kusini imekuja wakati Yanga ikiendelea na mipango ya kutafuta kocha mpya wa kuiongoza timu hiyo baada ya kuachana naye, huku klabu hiyo ikitarajiwa kumlipa mamilioni ya fedha kutokana na vipengele vya mkataba wao.

Katika taarifa iliyochapishwa na jarida la Sports With Daily News la Afrika Kusini, Manqoba amesema haamini matokeo mabaya ndiyo sababu pekee ya kuvunjwa kwa mkataba wake na Yanga, akidai kuna mambo mengine yaliyokuwa yakitokea nyuma ya pazia.

Manqoba Mngqithi


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons