Saida Karoli atunukiwa kiwanja na Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemzawadia kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 1,000 Msanii wa Muziki wa Asili, Saida Karoli.

Akizungumza katika Tamasha la Buhaya Festival lililofanyika Jijini Dar es Slsalaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema utaratibu wa kukabidhi kiwanja hicho kwa Msanii huyo unatarajiwa kufanyika Jumatatu, Oktoba 26, 2026.

Chalamila ametoa taarifa hiyo wakati akimwakilisha Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa katika tamasha hilo lililowakutanisha Wadau na Wapenzi wa Muziki wa Asili.

“Saida Karoli akiwa amealikwa pale JNICC, Mheshimiwa Rais aliniuliza jambo moja, Saida Karoli ni Mkazi wa Dar es salaam au wa Kagera? Kwa kweli nilisema sifahamu, lakini akawa ameniagiza baada ya kumwambia yupo hapa, akasema mtafutieni kiwanja Saida Karoli,” amesema Chalamila.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons