Singida Black Stars yakamilisha timu 4 makundi Afrika


Singida Black Stars imekuwa ni timu ya 12 kutinga hatua ya makundi ya CAF Confederation Cup msimu huu ikiwa ni baada ya kupata ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi ya Tusker FC .

Katika mchezo wa leo Singida Black Stars imetoshana nguvu na Tusker FC ya Kenya kwa kufungana bao 1-1 katika uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar.

Sasa ni rasmi kuwa timu zote nne zilizokuwa zinaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa msimu huu zimefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano yao.

Young Africans na Simba wapo makundi CAFCL na Azam FC pamoja na Singida BS wapo makundi CAFCC.