Mzize aipaisha Yanga
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu bara Yanga SC usiku huu imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo Yanga bado inakaa nafasi ya pili nyuma ya Simba SC, ikifanikiwa kufikisha pointi 22 huku ikizidi mchezo mmoja dhidi ya Simba ambao wapo kileleni na pointi 24.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Peter Shalulile dakika ya 22 na Clement Mzize dakika ya 77 ambaye goli lake ni la ushindi, Mashujaa FC wanaonolewa na Amani Josiah walianza kupata bao kupitia kwa Crispin Ngushi dakika ya 08.
Mechi inayofuata usiku huu ni JKT Tanzania na Dodoma Jiji.
