Simba yambakisha Dar Inno Loemba

Kiungo wa Simba SC “Inno Loemba” amesalia jijini Dar es Salaam licha ya kuonesha kiwango kizuri kwenye mchezo uliopita dhidi ya 15 De Agosto, huku wachezaji wengine waliosalia wakiwa ni pamoja na Vedastus na Kelvin Nashoni.

Uamuzi huu unakuja wakati kikosi cha Simba SC kikiwa kimeelekea mkoani Manyara kwa ajili ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate FC utakaopigwa kesho kutwa Alhamisi katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa.

Maneno mengi Yanasemwa hadi sasa kuhusu kiungo huyo fundi kutoka Congo Brazzavile, ambaye licha ya kutopewa nafasi mara kwa mara ndani ya kikosi cha Simba, lakini bado akiingia hata kwa dakika chache anaonyesha ubora mkubwa.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons