Simba kufanya uchaguzi Januari 3
Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba SC imetangaza kuhitisha mkutano mkuu wa dharula lakini pia imetangaza tarehe rasmi ya kufanya uchaguzi wa klabu hiyo.
Katika taarifa kwa umma, klabu hiyo imetoa tarehe ya kufanyika uchaguzi ambao ni tarehe 03, Januari mwaka 2027, sasa ulingo uko wazi kwa anayetaka uongozi hasa nafasi ya mwenyekiti na ujumbe wa Bodi.
