Azam FC yaifukuzia Yanga Ligi Kuu bara

Wauza lambalamba wa Azam FC usiku huu imeichakaza bila huruma timu ya Mbeya City ya mkoani Mbeya mabao 4-0 mchezo wa Ligi Kuu bara uwanjani wa Azam Complex Chamazi Dar es Salaam.

Mabao pekee ya Azam FC yamefungwa na Iddi Seleman Nado dakika ya 45, Feisal Salum Feitoto' dakika ya 62, Hassan Mubiru dakika ya 71 na Kipre Emmanuel Jr dakika ya 89, ushindi huo unaifanya timu hiyo kufikisha pointi 20 wakiwa na michezo 9 wakishika nafasi ya tatu.




Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons