Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2026

Tanzania, Kenya na Uganda kupokwa uenyeji AFCON

Picha
Hivyo Awali ilipangwa kufanyika nchini Kenya, Tanzania na Uganda, lakini mashindano hayo yanaweza kurudishwa au kuhamishiwa kwingine kutokana na kuchelewa kwa miundombinu na maandalizi. Inadaiwa CAF tayari imewasiliana na baadhi ya nchi zenye uwezo wa kuandaa mashindano hayo kwa muda mfupi: Morocco Algeria na Afrika Kusini . Ndani ya CAF, baadhi ya wajumbe wanadaiwa kuwa na matumaini madogo kuhusu nchi hizo tatu kuwa tayari kwa wakati. Hali hii inatofautiana na msimamo rasmi wa Rais wa CAF, Patrice Motsepe, ambaye amesema hakuna “Plan B wala Plan C” kwa AFCON 2027

Simba Queens mbabe wa Yanga Princess

Picha
Timu ya Wanawake wa Simba Queens imechomoza na ushindi wa 3-0 dhidi ya Yanga Princes kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii kwa upande wa Wanawake katika uwanja wa KMC Complex, Mwenge Dar es Salam. Simba Queens imetinga fainali ya michuano ya Ngao ya Jamii 2026 ambapo itachuana JKT Queens iliyotinga hatua hiyo kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Mashujaa Queens kwenye nusu fainali ya kwanza. Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Vivian Corozone, Senat Demise na Mary Siyame

Kaka yake Kibabage apandishwa cheo Marekani

Picha
Mogaj Kibabage, kaka wa mchezaji wa Simba SC, Nickson Kibabage, amepandishwa cheo kutoka Koplo (Corporal) hadi Sargent (Sergeant) katika Jeshi la Marekani (US Army). Mogaj amefanikiwa kupata cheo hicho baada ya kufaulu kozi maalumu ya kijeshi iliyomuwezesha kustahili kupandishwa cheo. Kupitia ukurasa wake wa Threads, Mogaj ametuma salamu kwa familia yake huku akiwashukuru kwa kumuombea na kumpa nguvu wakati wote alipokuwa akipitia mafunzo ya kozi hiyo. Hongera sana Mogaj Kibabage kwa hatua hii kubwa

Maagizo ya Waziri Makonda kwa viongozi wa Simba ni haya hapa

Picha
Katoka Kikao cha Waziri wa Michezo Paul Makonda na Viongozi wa Bodi ya Simba jambo kubwa ambalo wameelekezwa kufanya ni viongozi washirikiane, kila mtu atimize majukumu yake kwa maslahi ya taasisi. Kuanzia sasa tusisikie upande wowote ukishambulia upande mwingine. Iwapo ikitokea upande huo ndio hauna nia njema na klabu bali maslahi binafsi ameelekeza Waziri Wa Michezo kikao hicho kilichofanyika jana mchana katika hoteli ya Gran Melia Arusha.

Kagera Sugar yatambulisha benchi lake la ufundi

Picha
Klabu ya Kagera Sugar FC imemtangaza Amri Kiemba kuwa Kocha Msaidizi wa timu hiyo. Kiemba ambaye amewahi kuitumikia Kagera Sugar kama mchezaji ataenda kuungana na Kocha Mkuu Cedric Kaze, pamoja na Frank Domayo ambaye ametangazwa kuwa Kocha Msaidizi Namba Mbili. Katika hatua nyingine ya kuboresha benchi lake la ufundi, Kagera Sugar imemtangaza Kefa Mabadil kuwa Mchambuzi wa Video (Video Analyst) wa klabu hiyo. Benchi la Ufundi: ▪️ Cedric Kaze — Kocha Mkuu ▪️ Amri Kiemba — Kocha Msaidizi ▪️ Frank Domayo — Kocha Msaidizi Namba Mbili ▪️ Kefa Mabadala — Mchambuzi wa Video

Tanzania, Madagascar hakuna mbabe

Picha
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, jioni ya leo imeilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 timu ya taifa ya Madagascar mchezo wa kufuzu mataifa Afrika, AFCON zitakazofanyika baadaye mwakani katika ardhi ya Tanzania, Kenya na Uganda. Goli la Tanzania limefungwa na Cyprian Kachwele wakati goli la Madagastar lilifungwa na Fountaine, hata hivyo Taifa Stars imekosa mabao ya wazi hasa mshambuliaji wake Simon Msuva. Mechi nyingine ni kama ifuatavyo. FT: Burundi 2-2 Algeria FT: Lesotho 0-2 Morocco FT: Ethiopia 0-1 Senegal FT: Sudan Kusini 0-5 Misri FT: Comoros 1-0 Namibia Mechi nyingine ni. DAKIKA 70'  Cape Verde 1-2 Rwanda   Ghana 2-3 Gambia   Guinea-Bissau 2-0 Nigeria  Uganda 1-0 Libya  Zambia 1-0 Togo

Libasse Gueye kukosa dabi

Picha
Mshambuliaji wa klabu ya Simba Libasse Gueye huenda akaikosa dabi ya Kariakoo mnamo Oktoba 10, mwezi ujao. Ni baada ya kupata maumivu makali ya kifundo cha mguu akiwa mazoezini iliko kambi ya simba nchini afrika kusini Madaktari wanasema atakua nje kwa wiki 3 au 4 ili arejee tena

Edna Lema- Simba Queens ni mechi ngumu lakini?

Picha
Hakika tunakwenda kukutana na mchezo mgumu haiwezi kuwa mechi nyepesi sababu tuna wachezaji wapya kwenye timu yetu ila tuna faida ya kuwafahamu wapinzani wetu Simba Queens ili wao hawajui wachezaji wetu vizuri lakini sisi tunajiamini tuna timu nzuri ya kushindana msimu huu" "Wachezaji wetu wote wapo vizuri, hakuna majeruhi yoyote hadi sasa na hatuna sababu ya kusingizia kuelekea mchezo wetu wa kesho, benchi la ufundi wote tunataka kushinda" Edna Lema

Mwanariadha wa Tanzania apongezwa na Ubalozi Ujerumani

Picha
Mwanariadha wa Tanzania, Gabriel Geay amepokelewa na kupongezwa katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani baada ya kutwaa medali ya shaba katika mbio za BMW Berlin Marathon 2026. Geay amefikisha heshima hiyo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio hizo zilizofanyika Berlin Septemba 27, 2026, akiiwakilisha Tanzania katika moja ya mashindano makubwa ya marathon duniani. Akizungumza wakati wa kumpokea Geay, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Hassani Mwamweta amempongeza kwa matokeo hayo na kumtia moyo kuendelea na maandalizi ili kupambania nafasi ya kwanza katika mashindano yajayo. Mwamweta pia amesema amefanya mazungumzo na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusu kuongeza idadi ya wanariadha kutoka Tanzania watakaoshiriki mashindano ya kimataifa, ikiwemo BMW Berlin Marathon, hatua inayolenga kutoa nafasi zaidi kwa vipaji vya Tanzania kushindana kwenye majukwaa makubwa ya riadha.

Makonda awakutanisha vigogo Simba

Picha
Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, pamoja na Wajumbe wa Bodi wanaotokea upande wa Mo Dewji, wote wapo Arusha muda huu baada ya kupokea wito kutoka kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda. Leo Septemba 29, 2026, Waziri Makonda amewaita viongozi hao wa Simba SC kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea ndani ya klabu hiyo. Inaelezwa kuwa lengo la mkutano huo ni kujadili namna ya kupanga maendeleo ya soka nchini Tanzania, pamoja na kuhakikisha heshima na nidhamu ya mchezo wa soka vinaendelea kulindwa.

Kumbe Manqoba kaendeleza rekodi ya Mamelod

Picha
“Yote ninayoyafanya ndani ya klabu yangu hii mpya, Yanga SC, naona niko kwenye rekodi ya nyuma ya mwaka 2024, pale Afrika Kusini nikiwa na klabu yangu Mamelodi. Nilifanikiwa kupata alama zote kwa michezo mitano, hakuna mchezo niliopoteza, na hii sio mara ya kwanza kufanya vizuri. Pia nimekuja Tanzania, nimekuta ana muendelezo mzuri. Sikujali hilo, nikamfunga kwenye Ngao ya Jamii. Hivyohivyo tarehe 10, hakuna kitakachobadilika. Na uzuri, nilipata rekodi ya wenzetu ni namna gani wana uchungu na sisi, kwahiyo hatuna presha kabisa juu ya maendeleo yetu dhidi yao.”

Simba yageukia utalii Sauzi

Picha
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wapo ziarani nchini Afrika Kusini lakini wakiwa uko wametembelea mbuga ya wanyama na kujionea aina flani ya wanyama waliopo kwenye mbuga hiyo. Siku ya mapumziko na utalii kutembelea hifadhi ambayo ipo katika eneo ambalo tumeweka kambi hapa Afrika Kusini.

Kilichomuua Mzee Mpili chatajwa

Picha
“Baba aliamka asubuhi akiwa anajisikia vibaya sana tukakubaliana tumpeleke hospitali, lakini kuna mjomba wetu akatushauri tuanzie hospitali ya hapa hapa Ikwiriri maana Muhimbili ni mbali na mzee ana hali mbaya, hivyo tukampeleka hospitali ya hapa na ikawa ana upungufu wa damu hivyo ikashauriwa aongezewe damu , nikaambiwa watatoa damu yao halafu mimi niwatafute baadae watu wa kuja kurudisha damu ya watu. Akapimwa akagundulika damu yake ni group B, ikawa shida kidogo”. - Mtoto wa mzee mpili

Dkt Mwinyi apiga ziara ya ghafla mji wa AFCON

Picha
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi ametembelea mradi wa Mji wa michezo unaojulikana mji wa AFCON uliopo Fumba mkoa wa Magharibi B Unguja. Leo nimetembelea na kukagua Mradi wa Mji wa Michezo Zanzibar (AFCON), ikiwa ni sehemu ya ziara zangu za kawaida za kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali. Katika ziara hiyo, nimekagua miundombinu mbalimbali ikiwemo: • Uwanja wa mazoezi na uwanja wa mpira wa miguu — sehemu muhimu ya maandalizi ya miundombinu ya michezo. Mabwawa ya michezo — bwawa la kuogelea lenye urefu wa mita 50 pamoja na bwawa maalum kwa mchezo wa kuruka majini (Diving Pool). Fan Zone — eneo la wazi lenye uwezo wa kuhudumia watu 4,000. Miundombinu ya bandari — inayojengwa kwa ajili ya kuhudumia boti ndogo na kubwa. Awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika tarehe 31 Desemba 2026, hatua itakayoiwezesha Zanzibar kuwa miongoni mwa wenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Wachezaji wawili wapewa kadi nyekundu baada ya kumvuta nywele nyota wa Anguilla

Picha
Mchezaji wa timu ya taifa ya Anguilla, Aedan Scipio, mwenye umri wa miaka 36, amekuwa gumzo baada ya wachezaji wawili wa timu ya taifa ya Antigua na Barbuda kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumvuta nywele katika mchezo wa jana. Scipio, anayefahamika kama moja ya wachezaji wenye nywele ndefu zaidi katika soka, aliingia uwanjani akitokea benchi la akiba, lakini baadaye akavutwa nywele mara mbili na wachezaji wa timu pinzani. Wachezaji hao wawili wa Antigua na Barbuda walionyeshwa kadi nyekundu moja kwa moja kwa matukio hayo, licha ya timu yao kuwa inaongoza kwa mabao 5-0. Kwa namna ya kipekee, nywele za Scipio zikawa gumzo na kuibua tukio lililobadilisha mwelekeo wa mchezo, huku kadi nyekundu mbili zikitolewa kwa sababu hiyo hiyo

Tutabeba ubingwa wa bara- Barker

Picha
Kocha Barker akielezea umuhimu wa kambi ambayo tumeiweka Afrika Kusini na ushirikiano mkubwa ambao anatoa Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji, kwa kikosi chake, ikiwepo kulipa gharama zote za kambi hii. “Nahitaji kuondoka Simba SC nikiwa nimeipa ushindi ambao haujawahi kupatikana kwa takribani misimu 5. Nahitaji kuifanya iwe ya mfano ndani ya ligi ya Tanzania. Msimu uliopita nilipata nafasi ya kufanya vizuri, licha ya timu nilikuta ikiwa katika nyakati mbovu. Ila kwa msimu huu, Mungu asaidie tu, maana nilichopanga ni kuwafanya mashabiki wa Simba SC waongezeke, hata wale waliokata tamaa wanaweza kurudi. Uwezo wangu mimi naujua, si kama wao, kila mtu ana uwezo wake. Ndiyo maana kila timu ina shida zake. Nahitaji kufanya jaribio la mechi za kirafiki hapa nchini Afrika Kusini kwa kipindi tulichoweka kambi huku. Mimi niseme Rais wetu amejua nini tunahitaji, ndiyo maana tumepewa heshima ya kupewa kambi mbali na Tanzania. Huu ni mwanzo mzuri kabisa. Lile kombe moja tulilobeba sio kwamba ndiyo tu...

Mzee Mpili afariki dunia

Picha
UONGOZI wa Young Africans Sports Club (Yanga SC) umetangaza kwa masikitiko kifo cha mwanachama wake, Haji Omari Ramadhani Mpili, maarufu kama Mzee Mpili, kilichotokea usiku wa Septemba 27, 2026. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, marehemu Mpili alifariki dunia katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani, alipokuwa akipatiwa matibabu. Uongozi umeeleza kuwa maziko yanatarajiwa kufanyika leo, Septemba 28, 2026, majira ya saa 10:00 jioni. Shughuli za maziko zitafanyika katika Makaburi ya Msikiti Mkubwa yaliyopo Wilaya ya Ikwiriri, Mkoa wa Pwani. “Uongozi wa Young Africans Sports Club unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa mpira, na kuwaomba kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amina,” imeeleza taarifa hiyo.

TFF yapata Katibu Mkuu mpya

Picha
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtangaza Evans Mgeusa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Shirikisho hilo, akichukua nafasi ya Oscar Mirambo aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo. Kabla ya uteuzi huo, Mgeusa alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Njombe (NIOREFA). Aidha, Oscar Mirambo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu, huku Mustapha Yusuph akiteuliwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Fedha wa TFF.

Amri Kiemba kocha msaidizi Kagera Sugar

Picha
Kiungo wa zamani wa timu za Simba SC, Yanga SC, Azam FC, Kagera Sugar pamoja na Timu ya Taifa (Taifa Stars) na mchambuzi maarufu wa soka, Amri Kiemba, amejiunga rasmi na benchi la ufundi la klabu ya Kagera Sugar kama Kocha Msaidizi kwa msimu wa 2026/2027. Kiemba tayari anao uzoefu wa benchi la ufundi, ambapo aliwahi kuhudumu kama Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) chini ya kocha Hemed Selemani 'Morocco'. Kiemba anarejea Kagera Sugar ambapo aliwahi kuichezea hapo awali akiwa mchezaji, Na tayari amesharipoti kambini na kujiunga na kikosi kwa ajili ya maandalizi ya michezo inayofuata.