Miss Grand International uso Kwa uso na watu wa mitandao
Miss Grand International 2026, Jihan Dimachk, akiwa na baadhi ya vijana na washawishi wa mitandao ya kijamii waliompa ushirikiano kwa kumpigia kura, katika viunga vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma leo, Jumatano, Oktoba 28, 2026.
Jihan na vijana hao wamepata mwaliko wa kuhudhuria kikao cha Bunge na kushuhudia shughuli zake moja kwa moja, ikiwa ni siku ya pili ya Mkutano wa Tano wa Bunge la 13.



