Mashabiki wamrudisha Ramovic, Yanga

Baada ya klabu ya Young Africans kumfuta kazi kocha mkuu Manqoba Mngqithi, sasa imeanza kutafuta chaguo sahihi la kocha bora ambaye anaweza kuipa ubingwa wa CAF pamoja na Ligi Kuu ya NBC.

Mashabiki wa Young Africans wameomba chaguo sahihi kutoka kwa kocha Sead Ramović, mwenye uraia wa Ujerumani, kurejea klabuni hapo kama kocha mkuu.

Taarifa zinadai kuwa kocha huyo kwa sasa amepokea ofa mbili kutoka vilabu mbalimbali, ikiwemo Yanga SC pamoja na klabu moja kutoka Saudi Arabia.

Kwa sasa, Sead Ramović ana jukumu la kuchagua pendekezo gani analoweza kulikubali na kuanza kazi mara moja. Kwa upande wa Yanga, lengo ni kumpata kocha sahihi.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons