Mayele aipeleka makundi Al Ahli
Klabu ya Al Ahly Tripoli ya Libya ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya CAF Confederation Cup baada ya kuiondosha Welwalu Adigrati kwa aggregate ya mabao 8-1.
Kabla ya kuiondosha Welwalu, Al Ahly Tripoli waliiondosha KMKM ya Zanzibar kwenye raundi ya kwanza ya awali kwa aggregate ya mabao 7-0.
Kwahiyo, Al Ahly Tripoli kwenye kampeni yao ya kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho msimu huu wamefunga jumla ya mabao 15 na kuruhusu bao 1 pekee.
Fiston Mayele amefunga jumla ya mabao 4 kwenye kampeni hiyo..!
