Aliyekuwa Katibu Mkuu wa shirikisho la soka nchini, Michael Wambura, ambaye anapinga kuenguliwa katika uchaguzi mkuu wa Klabu ya Simba, amesema atamburuza Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Simba, Damas Ndumbaro, kwenye Kamati ya Maadili ya TFF kufuatia 'kumpakazia' kashfa ya kughushi nyaraka na pia kumtukana. Wambura alisema katika taarifa yake aliyoitoa kwa waandishi wa habari jana kuwa anawasilisha malalamiko yake katika Kamati ya Maadili ya TFF ili ukweli wa mambo ufahamike. "Kwa kuwa nimeshakata rufaa TFF kupinga maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba, busara inanielekeza kutolumbana na na kujibizana na Ndumbaro ili kuipisha Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF ifanye maamuzi yake," alisema katika taarifa yake hiyo. Aliongeza: "Kwa mambo ambayo hayana uhusiano na uchaguzi kama kughushi nyakara, matusi na kashfa mbalimbali mambo hayo nitayawasilisha kwa Kamati ya Madili ya TFF ili ukweli ufahamike na hatua zichukuliwe na baada ya hapo vyombo vya dola vinavyo...