PODOLSKI KUIKOSA ALGERIA LEO
Mshambulizi wa Ujerumani na
Arsenal ya Uingereza Lukas Podolski hatoweza kushiriki mechi ya mkondo
wa pili kati ya Ujerumani na Algeria iliyoratibiwa kuwa Porto
Alegre.
Sasa madaktari wa timu hiyo inayopigiwa upatu kufuzu kwa fainali ya kombe la dunia mwaka huu wanasema kuwa anahitaji angalau siku mbili au tatu kupumzika ilipaja lipate nafuu na hiyo inamaanisha kuwa kocha Joachim Loew
sasa atalazimika kumchezesha mshambulizi mwengine upande wa kushoto .
Kikosi cha Loew kingali kinasuri habari kumhusu kiungo wa upande wa kulia Jerome Boateng ambaye pia hakuweza kushiriki mazoezi yao ya mwisho kutokana na jeraha la goti.
Ujerumani itachuana na the Desesrt Foxes ya Algeria jumatatu katika uwanja wa Porto Alegre’s Beira-Rio .