KWAHERI LAMPARD, ANAONDOKA CHELSEA
KIUNGO Frank Lampard anaondoka Chelsea baada ya kuitumikia kwa miaka 13 na klabu hiyo sasa inaisaka saini ya Cesc Fabregas arithi mikoba.
Kiungo huyo mkongwe huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 35 anatarajiwa kwenda kumalizia soka yake katika Ligi Kuu ya Marekani kwenye klabu ya New York City.
Fabregas anaweza kuuzwa na Barcelona kwa Pauni Milioni 30 na klabu yake ya zamani, Arsenal haijaonyesha dhamira haswa ya kumrejesha, jambo ambalo linaifanya Chelsea ibakie kuwa katika nafasi ya kumnasa Mspanyola huyo.
Lampard, ambaye atakuwa Nahodha wa England kesho ikimenyana na Ecuador Uwanja wa Sun Life, amesema daima ataikumbuka Chelsea; ‘Nyumbani kwangu na moyoni kwangu’.
Katika taarifa yake ya kuaga jana, Lampard hakumtaja Jose Mourinho — mtu ambaye wakati wote amekuwa akimsifu kama kocha bora duniani — kwa jina.
Mkataba wa Lampard Chelsea uliokuwa unamfanya alambe mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki unamalizika Juni 30 na anajiandaa kukubali ofa ya kucheza Marekani.
Mchezaji huyo aliyefunga mabao 211 Chelsea tangu ajiunge nato kutoka West Ham mwaka 2001 na kushinda nayo mataji matatu ya Ligi Kuu ya England, manne ya Kombe la FA na moja la Ligi ya Mabingwa, anatarajiwa kutangaza kustaafu soka ya kimataifa baada ya Kombe la Dunia.