MESSI AIONGOZA ARGENTINA KUSHINDA 2-1 KWA MBINDE KOMBE LA DUNIA

ARGENTINA imeanza vyema Kombe la Dunia baada ya usiku wa jana kuilaza Bosnia-Herzegovina mabao 2-1 katika mchezo wa Kundi Kombe la Dunia Uwanja wa Maracana mjini  Rio de Janeiro, Brazil.


Shukrani kwake Mwanasoka bora wa zamani wa dunia, mshambuliaji wa Barcelona ya Hispania, Lionel Messi aliyefunga bao la pili la Argentina dakika ya 65 akimalizia pasi ya Gonzalo Higuain.
  
Sead Kolasinac aijifunga dakika ya tatu katika harakati za kuokoa kuipatia Argentina bao la kwanza kabla ya Vedad Ibisevic kutumia pasi ya Senad Lulic kuisawazishia Bosnia dakika ya 84.

Kikosi cha Argentina kilikuwa; Romero, Campagnaro/Gago dk45, Fernandez, Garay, Zabaleta, Maxi Rodriguez/Higuain dk45, Mascherano, Di Maria, Rojo, Messi na Aguero/Biglia dk86.

Bosnia-Herzegovina; Begovic, Mujdza/Ibisevic dk70, Bicakcic, Spahic, Kolasinac, Besic, Hajrovic/Visca dk72, Pjanic, Misimovic/Medunjanin dk74, Lulic na Dzeko.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA