MAMBO UWANJANI TV: MAJIBIZANO TOKA VIJIWENI
Mhariri wa mtandao huu Exipedito Mataruma amesema mipango yote imekamilika na kuanzia sasa maandalizi tu ndio yameanza, 'Muda mrefu mrefu Blogu yetu ilikuwa katika malengo ya kuanzisha kipindi chake cha Tv na sasa tunataraji kuanza', alisema Mataruma.
Kipindi hicho kitarushwa kwa rekodi ila mambo yakikamilika kitakuwa live, Mataruma aliongeza kwa kudai lengo la kufanya hivyo ni kukaa karibu na watazamaji wake ambao wanataka habari murua kutoka kwao, tayari vifaa kwa ajili ya kurekodi vinawasili na muda wowote kipindi kitakuwa hewani