THOMAS MULLER WA UJERUMANI AITOA KAMASI URENO NA RONADLO WAO, AANDIKISHA REKODI MPYA YA HAT TRIK
Nyota huyo wa Bayern Munich alifunga bao la kuongoza dakika za mapema kwa mkwaju wa penati na kuwapa mwanzo mzuri katika uwanja wa Arena Fonte Nova wana nusu fainali hao wa mwaka 2010 nchini Afrika kusini.
Mabao ya Muller usiku huu yalifungwa katika dakika za 12 (penati), 45, 78, na goli lingine lilifungwa na beki wa kati Mats Hummels katika dakika 32.
Ureno walipata majanga baada ya mshambuliaji wake wa kati Hugo Almeida na Fabio Coentrao kupata majeruhi, lakini mbaya zaidi walishuhudia beki wao wa kati Pepe akitolewa nje kwa kadi nyekundu wakati timu yake iko nyuma kwa mabao 2-0 baada ya kumfanyiwa madhambi Muller.
Bahati yenu hapa hayupo Ramos wala Gareth Bale
Kikosi cha Germany: Neuer 6; Boateng 6, Mertesacker 6, Hummels 7 (Mustafi 73min, 6), Howedes 6, Lahm 7; Khedira 7.5, Kroos 6; Muller 8 (Podolski 80), Ozil 5.5 (Schurrle 63, 6.5), Gotze 7.
Kikosi cha Ureno: Patricio 5.5; Pereira 5, Alves 5, Pepe 2, Coentrao 4.5 (A Almeida 65, 5.5); Moutinho 5, Veloso 5 (Costa 45, 5), Meireles 5; Nani 6, H Almeida 5 (Eder 23, 5), Ronaldo 5.
Wachezaji wa akiba: Eduardo, William Carvalho, Vieirinha, Luis Neto, Rafa, Varela, Ruben Amorim, Postiga, Beto.
Kadi ya njano: Pereira.
Kadi nyekundu: Pepe.
Mchezaji bora wa mechi: Thomas Muller.
Mwamuzi: Milorad Mazic (Serbia)
Katika mchezo mwingine wawakilishi wa Afrika, Nigeria walitoshana nguvu na Iran ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo mwingine mkali