HAMOSNOTA KUIBUKIA IDD NA ZAWADI YA MAMA

Na Prince Hoza

MSANII chipukizi anayekuja kasi kwa sasa ambaye anatamba na wimbo wake wa 'Bye bye' Hashimu Momba 'Hamosnota' ameamua kumletea zawadi ya Idd mama yake mzazi lakini mashabiki wake ndio watakaoipokea siku ya sikukuu ya Idd el fitr.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni, Hamosnota amesema anatarajia kuitambulisha nyimbo yake mpya iitwayo 'Safari kwa mama' ambapo ataiachia siku ya sikukuu ya Idd El Fitr.'Ifikapo Idd El Fitr nitaachia wimbo mpya unaokwenda kwa jina la 'Safari kwa mama' nimeamua kutunga wimbo huu kwa ajili ya wale wanawake wanaokwenda mara kwa mara kwa mama zao wakati wakiwa ndani ya ndoa', alisema na kuongeza.




Hamosnota akiwa ameweka pozi

'Unajua ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu hii mtu ameshaolewa lakini haifiki mwezi utasikia kaenda kwa mama yake sasa hapo ndoa hakuna', alisema msanii huyo ambaye kimuonekano ni sharobalo kidogo.

Aidha ameelezea malengo yake mengine ni kujitangaza zaidi kupitia mitandao ya kijamii ambapo anatarajia kuachia wimbo wake huo youtube, kipindi hiki cha mwezi mtukufu Ramadhani Hamosnota amesimamisha shoo zake ili kuungana na waislamu wote katika mfungo huo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA