WEMA AKANA UJAUZITO WA DIAMOND

Sina ujauzito wa Diamond nyie nani kawaambia
Baada ya stori nyingi kuzagaa kuwa mwigizaji na mpenzi halali wa mwanamuziki wa bongo fleva Diamond Platinumz – Wema sepetu kuwa yu mjamztio wa wiki 7 na mimba ya msanii huyo, hatimaye jana mwanadada huyo ameamua kufunguka “exclusively” kwenye mtandao mmoja wa kijamii na kujibu habari hizo akisema haya yafuatayo kuwa hajabahatika kuwa na ujauzito.


“Jamani hizi habari za mimi kuwa pregnant (mjamzito).... sijui watu wanatolea wapi... Im NAT (NOT)... Dah... I wish I was... But im nat wapenzi wangu..”

Akimaanisha kuwa yeye sio mjamzito ila anatamani sana sana awe na ujauzito huo lakini kwa sasa yeye bado.!

Ameongeza kuwa anatamani hali hiyo imtokee lakini bado na anashangaa kwanini watu wanaeneza taarifa kuwa yeye yu mjamzito.

Wema ambaye kwa sasa penzi lake na Diamond limevunja rekodi ya lile la kwanza kabla halijavunjika na baadaye kurudiana tena, amejikuta akizushiwa kuwa ana ujauzito wa Diamond.

Naye Diamond amekuwa anatamani siku moja kupata mtoto na ikafikia hatua ya kutunga wimbo wake unaoelezea kifo ambapo katika mashairi yake amesema atakufa bila mtoto na kila anayekutana naye kimapenzi amekuwa akimwambia subiri muda haujafikia.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA