FILIPPO INZAGHI KOCHA MPYA AC MILAN

Enzi zake Inzaghi akisakata soka, sasa ni kocha mpya AC Milan
AC Milan imemfuta kazi mkufunzi wake Clarence Seedof baada ya kuhudumu kwa chini ya miezi 5 na kumtangaza Filipo Inzaghi kama kocha mpya.


Seedof mwenye umri wa miaka 38 alikuwa amechukua nafasi yake Massimiliano Allegri mwezi Januari, wakati timu hiyo ilikuwa katika nafasi ya 11 katika ligi kuu ya Italia Serie A na alama 30 nyuma ya viongozi wa wakati huo Juventus, ambao walishinda taji hilo mwisho wa msimu.
Kocha mpya wa AC Milan Filipo Inzaghi akipungia mashabiki waliomlaki

Hata hivyo, mholanzi huyo alishindwa kubadili mkondo na msururu wa matokeo duni uliendelea hadi mwisho wa msimu timu hiyo ilipomaliza ikiwa na alama 45 nyuma ya mabingwa msimu huu Juventus.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA