JK AIFARIJI FAMILIA YA MZEE SMALL

Na Mariamu Libibo

RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete jana aliwaongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kumzika aliyekuwa msanii maarufu wa maigizo nchini Said Ngamba kwa jina maarufu Mzee Small Wangamba yaliyofanyika katika makaburi ya Tabata Segerea.


Rais Kikwete alienda msibani nyumbani kwa marehemu Tabata Kisiwani na kuwafariji wafiwa ambapo pia alizungumza na familia ya marehemu, haijawahi kutokea kwa Tanzania kutembelewa na rais hasa kwenye misiba ya wasanii na wanamichezo.

Lakini Rais Kikwete akiongozwa na walinzi wake alishiriki katika mazishi ya msanii huyo mkongwe ambaye alikuwa akisumbuliwa kwa muda mrefu, mbali ya Kikwete kuudhuria msiba huo wasanii mbalimbali nchini nao walishiriki katika mzishi hayo ya msanii huyo mkongwe ambaye anatajwa kama muasisi wa sanaa ya maigizo nchini.


Kikwete pia alitembelea nyumbani kwa marehemu Kanali Hassan Mwanakatwe ambaye alifariki dunia hivi karibuni na anatarajia kuzikwa leo Jumanne, hii ni mara nyingine kwa Rais Kikwete kuudhuria misiba ya mastaa mbalimbali hapa nchini na amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara.

Mtandao huu unawapa pole familia za Hassan Mwanakatwe na Mzee Small kufuatia vifo vya watu hao maarufu hapa nchini ambao walipigana kwa nguvu zao lakini vifo vimeondoa uhai wao

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA