UKICHEZA SIMBA AU YANGA NDIO UNACHAGULIWA TAIFA STARS- CASILAS

Na Prince Hoza

MLINDA lango wa kutumainiwa wa timu ya Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani mkoani Morogoro Hussein Sharrif 'Cassilas' ambaye pia ndiye kipa bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (2013/14) ameponda kauli zinazotolewa na wadau wa soka hasa baada ya yeye kutangazwa kipa bora.

'Mimi ndio kipa bora lakini siwezi kuitwa Stars labda niwe Simba, Yanga au Azam', anasema Casilas.


Casilas amelaani vikali baadhi ya wadau kuponda uteuzi wake wa kuwa kipa bora msimu uliomalizika wakati hayupo kwenye timu ya taifa, Taifa Stars.

Hivi karibuni mchambuzi wa soka na mdau maarufu Joseph Kanakomfumo amebeza uteuzi wake wa kuwa kipa bora wakati hayupo Stars, Kanakomfumo ameshangazwa na uteuzi huo na kudai imekuwa mara kwa mara kutoa tuzo kwa wasiostahili.

Lakini mlinda lango huyo ameipuuza kauli hiyo ya Kanakomfumo ambaye pia ni kocha kitaaluma, Casilas amedai kuwa kuna kasumba katika uteuzi wa timu ya taifa, Taifa Stars tena imeendelea kukithili.

Amesema ili uitwe timu ya taifa basi ni lazima uwe mchezaji wa Simba, Yanga au Azam fc, hivyo inawawia vigumu wachezaji kama wao kuonekana bora.'Nastahili kuwa kipa bora, lakini kuitwa kwenye timu ya taifa labda nichezee Simba, Yanga au Azam', alisema na kuongeza.

'Yamekuwa mazoea ya kuteua kikosi cha timu ya taifa kwa kufuata timu zenye majina makubwa ambazo ni Simba, Yanga na Azam fc, ila kama wangejali ubora wa mchezaji husika nasi wasingepata taabu kwani tupo kibao huku Mtibwa na kwingineko', aliongeza kipa huyo aliyelamba kitita cha shilingi Mil 5.

Kipa huyo ameponda uteuzi wa timu ya taifa ambaounatokana na majina na si uwezo wa mchezaji, na ndio maana maendeleo ya soka nchini yanadolola kutokana na uduni wa wachezaji.

Na ili timu ya taifa iungwe mkono na wengi basi ni bora wachezaji wakatokea Zimba, Yanga au Azam, kwani timu hizo tayari zimeota mizizi kwa mashabiki wengi wa soka nchini, Casilas anawaniwa vikali na Simba ingawa timu yake ya
Mtibwa imegoma kumuuza.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA