WAMBURA AMSHANGAA NDUMBARO KUMFUTA SIMBA
Na Prince Hoza
ALIYEKUWA mgombea wa nafasi ya urais katika klabu ya Simba Michael Richard Wambura ambaye alirejeshwa hivi karibuni na kamati ya rufaa ya TFF, amemshangaa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba wakili Damas Daniel Ndumbaro kwa kumfuta kabisa katika nafasi huyo wakati yeye akiwa ajarejeshwa rasmi.
Wambura anasema, Ndumbari vipi tena: mimi nilishaenguliwa na kamati yako nashangaa kunifuta kabisa, wapi?
Wambura amecheka kwanza kisha akasema, Ndumbaro si mwadilifu katika taaluma yake na ndio maana aliwahi kumwambia aende tena darasani, 'mimi sijarejeshwa rasmi katika kinyang'anyiro hicho nashangaa anatangaza mbele ya waandihsi amenifuta', alisema Wambura.
'Ninachofahamu kwa sasa uchaguzi huo umesimamishwa na TFF kupitia rais wake Jamal Malinzi na pia mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage ametangaza kuifuta kamati hiyo hivyo kunifuta mimi ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu', aliongeza.
'Hadi sasa sijapewa barua ya kurudishwa katika uchaguzi huo na kamati ya TFF wala yeye (Ndumbaro) ajapewa barua kuwa mimi nimerejeshwa, kiungwana angesubiri barua kwanza kisha akatangaza hayo', aliendelea kusema Wambura.
Wambura amedai yeye kwa sasa anachotambua ameenguliwa na kamati ya Ndumbaro ila kesi yake imeshazungumzwa baada ya kukata rufaa anachosubiri ni barua yake kama amerejeshwa au laa.
Kwa maana hiyo uchaguzi wa Simba huenda usifanyike huku mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage akiendelea kupeta madarakani.