HAPANA CHEZEA CRISTIANO RONALDO, AIONGOZA URENO KUUA MTU YANGA

ILIMCHUKUA sekunde 52 Cristiano Ronaldo kuithibitishia dunia kwamba amepona na yuko fiti kwa Fainali za Kombe la Dunia wakati Ureno ikiitandika Jamhuri ya Irelando mabao 5-1 jana katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa MetLife.


Akiwa hajacheza mechi tangu baada ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi uliopita, Ronaldo aliwatoka mabeki wa Ireland baada ya kugusa mpira kwa mara ya kwaza na kufumua shuti lililolenga lango. Ulikuwa ujumbe tosha CR7 amerejea.

Mbele ya Roy Keane, mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United, aligongesha mwamba, alitoa pasi, na mara mbili akakaribia kufunga na hakika alionyesha kabisa yuko tayari kwa kipute cha Brazil.

Mabao ya Ureno yalifungwa na Hugo Almeida dakika za tatu na 37, Richard Keogh alijifunga dakika ya 19 na Vierinha dakika ya 77 na Fabio Coentrao na bao pekee la Ireland lilifungwa na McClean dakika ya 52.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA