WAGENI WASITISHA MGOMO BRAZIL
Vuguvugu la watu wasio na
makaazi nchini Brazil ambalo limekuwa likiunga mkono maandamano ya
kupinga kombe la dunia sasa wametangaza kuwa wamesitisha maandamano hayo
muda wote wa dimba hilo.
Kama kweli wakiendeleza vitisho hivyo basi itakuwa kasheshe kubwa mashabiki kusafiri hadi viwanjani kujionea mechi walizokuwa wakizisubiri kwa hamu kuu.
Mechi ya ufunguzi hapo kesho ni kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia.
Maandalizi ya kombe la dunia ya Brazil yamekubwa na chelewachelewa na pia migomo ya makundi mbalimbali yanayotumia fursa hiyo ya kombe la dunia kudai nyongeza za mishahara na huduma bora za kijamii kutoka kwa serikali inayoshtumiwa kwa ufisadi na matumizi makubwa katika ujenzi wa viwanja na miundo mbinu kwa ajili tu ya kombe la dunia.