KANISA LAWATAKA WAUMINI WAKE KUFANYA MAZOEZI YA VIUNGO

Na Mariamu Libibo

UTAIPENDA tu: Kanisa la wasabato lililopo Tabata Mbuyuni jirani na maghorofa ya NSSF Aroma jijini Dar es Salaam limewataka waumini wake kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuondokana na ugonjwa wa saratani ya matiti na kupunguza uzito wa mwili.

Mazoezi ya viungo yanasaidia kupunguza uzito pamoja na maradhi ya saratani ya matiti kwa akina mama, amesema Mtoa mada hayupo pichani

Wito huo umetolewa jana wakati mtoa mada akiwaelimisha waumini wa dhehebu hilo wakiwemo wamama na wababa waliofurika kumsikiliza mtoa mada huyo, aliwataka waumini hao kufanya mazoezi ya viungo kila siku ili kuondokana na maradhi ya saratani ya matiti inayoenea kwa kasi hapa nchini.


Pia amewataka kufanya mazoezi kwa ajili ya kupunguza uzito ambao hupelekea unene (Obbesite) na kupunguza mafuta machafu (Corestol) husababisha maradhi ya kisukari, presha na moyo, amewataka kufanya mazoeiz ya kukimbia au kuruka kamba kila siku kwani kufanya hivyo kutawasaidia.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA