ETO'O AENDELEZA VITA YAKE NA MOURNHO

MSHAMBULIAJI Samuel Eto'o jana amerudia kushangilia kama kikongwe baada ya kuifungia Cameroon bao la kuongoza ikitoka sare ya 2-2 na Ujerumani katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na Kombe la Dunia.


Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33 alimtoka beki Mats Hummels kuuwahi mpira kabla ya kumtungua kipa wa Ujerumani, Roman Weidenfeller dakika ya 62.

Eto'o, alishangilia kama hivyo awali katika klabu yake Chelsea baada ya kufunga dhidi ya Manchester United katika Ligi Kuu ya England, kujibu mapigo ya kocha wake, Mreno Jose Mourinho aliyehoji umri wake akidai ni mkubwa kuliko miaka anayotaja.

Bao lingine la Cameroon lilifungwa na Choupo-Moting dakika ya 78, wakati mabao ya Ujerumani yalifungwa na Muller dakika ya 66 na Schurrie dakika ya 71.

Kikosi cha Ujerumani kilikuwa: Weidenfeller, Boateng, Mertesacker, Hummels, Durm/Howedes, dk85, Khedira/Kramer, dk73, Kroos, Muller, Ozil/Podolski, dk63, Reus, Gotze/Schurrle, dk58.

Cameroon: Itandje, Djeugoue, Bedimo/Assou-Ekotto, dk58, N'Koulou, Song, Mbia/N'Guemo, dk46, Enoh, Matip, Choupo-Moting, Moukandjo, Eto'o/Webo, dk90.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA