AZAM FC YAZIVUTIA KASI YANGA, TP MAZEMBE

Azam FC's photo.Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Azam Fc leo wameanza Rasmi mazoezi ya kujiandaa na ligi kuu Tz Bara pamoja na Mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika, hizo ni salamu kwa Yanga ambao ni washindi wa pili wa ligi kuu Tanzania bara na wawakilishi wa michuano ya kombe la shirikisho mwakani.

Pia Yanga watakutana nayo Agosti katika mechi ya ngao ya hisani, mwaka jana timu hizo zilikuatana katika mechi kama hiyo na Azam ilikubali kichapo cha bao 1-0 hivyo mwaka huu haitakubali kufungwa na ndio maana wameingia kambini upesi.


Aidha Azam mwakani itashiriki ligi ya mabingwa barani Afrika hivyo inaweza kujikuta inapangiwa na miamba kama TP Mazembe, Al Ahly au Enyimba International, kuanza mazoezi mapema kunapelekea ufiti kwa nyota wake na kufanya vizuri katika ligi na michuano ya kimataifa.

Mazoezi hayo yamefanyika kwenye uwanja wake uliopo chamazi jijini Dar es salaam chini ya kocha msaidizi Kalimangonga Ongala, Ibrahim Shikanda, Iddy Cheche pamoja na kocha wa Makipa Iddy Abubakari.

Kocha mkuu Joseph Omog anatarajia kujiunga na timu tarehe 20/6/2014. Azam Fc Mapinduzi ya kweli katika soka

 Azam FC's photo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA