ROBBEN AKIRI KUJIANGUSHA KUMDANGANYA REFA AWAPE PENALTI UHOLANZI

WINGA Arjen Robben alijaribu kumdanganya refa katika mchezo wa 16 Bora jana Kombe la Dunia, Uholanzi ikiifunga mabao 2-1 Mexico na kwenda Robo Fainali.

Mholanzi huyo alisema kwamba alijirusha kutafuta penalti, lakini lie iliyotolewa dakika ya tatau ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida, ambayo Uholanzi waliitumia kusonga mbele katika mbio za kukimbilia Kombe la Dunia.


Robben aliomba penalti mbili zilizokjataliwa mapema katika mchezo huo - kabla ya Klaas Jan Huntelaar kufunga dakika za majeruhi bao la ushindi - na baadaye akaomba radhi kwa kujaribu kutaka kumdanganya refa Mreno, Pedro Proenca.

"Lazima niombe radii "amesema Robben. "Moja [mwishoni] ilikuwa penalti, lakini nyingine zile zilikuwa za kujirusha kipindi cha kwanza. Nisingefanya hivyo.'

Robben alipewa penalti ya dakika za lala salama baada ya kuangushwa na Nahodha wa Mexico, Rafael Marquez, lakini nyota huyo wa Bayern Munich awali alikataliwa matatuta mawili aliyolilia, wakayti timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1-0.

Baadaye Uholanzi ikasawazisha, zikiwa zimebaki dakika tatu mchezo kumalizika kupitia kwa Wesley Sneijder na katika dakika za majeruhi, Robben akaangushwa katika penalti iliyokubalika na Huntelaar akaifungia timu hiyo bao la ushindi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA