MAPOPO FC YAZIDI KUCHANJA MBUGA CHALINZE

TIMU ya soka ya Mapopo FC ya Mdaula Chalinze mkoani Pwani (Pichani nikikosi cha Mapopo FC) imezidi kuchanja mbuga katika michuano ya kuwania mbuzi mnyama baada ya kuilaza timu ngumu ya Majengo FC mabao 2-0 katika uwanja wa shule ya Mdaula.


Washindi walijipatia magoli yao yaliyofungwa katika vipindi vyote viwili na mshambuliaji Mohamed Diku na lingine likifungwa na Muna 'Sanchez'.

Licha ya ushindi huo, Mapopo walipoteza nafasi nyingi za kufunga na zikiwa za wazi ambapo mshambuliaji wake Mohamed Diku akipoteza nafasi mbili akiwa yeye na goli.

Hadi mwisho wa mchezo Mapopo imeibuka kidedea, hadi sasa Mapopo inaongoza ligi hiyo inayoshirikisha timu 7 na moja tu ndio inaaga mashindano na kubakia sita ambazo zitacheza hatua ya sita bora, Mapopo imecheza mechi tano na kushinda zote.

Mapopo ilizifunga Young Bad 3-2, Veterani 4-1, Chalinze 2-0, Bodaboda FC 4-2 na Majengo FC 2-0, Wakati huo huo Mapopo FC imepokea mwaliko wa kushiriki michuano ya kuwania jezi yatakayofanyika Chalinze.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA