Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2018

MAAFANDE WA JKT TANZANIA YAWAPIGISHA KWATA PRISONS KWAO

Picha
Na Exipedito Mataruma. Mbeya Timu ya JKT Tanzania inayonolewa na Bakari Shime "Mchawi mweusi", imefanikiwa kuichapa Tanzania Prisons mabao 2-0 uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mechi ikipigwa mchana. JKT Tanzania iliyopanda Ligi Kuu bara imeweza kutinga nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup baada ya ushindi huo wa leo ambapo sasa itaumana na mshindi kati ya Yanga Sc na Singida United itakayopigwa kesho. Mabao ya washindi yametiwa kimiani na Ally Ahmed dakika ya 13 kipindi cha kwanza na Hassan Matelema dakika ya 78 kipindi cha pili, mchezo mwingine wa robo fainali ya michuano hiyo itapigwa usiku wa leo kati ya Azam Fc na Mtibwa Sugar uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam JKT Tanzania imeifunga Prisons 2-0

FEI TOTO ANAKWENDA YANGA

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kiungo mahiri wa JKU na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes pamoja na Taifa Stars, Fesal Salum "Fei Toto" anakaribia kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga Sc iwapo itampa dau analotaka. Taarifa zenye uhakika zilizotufikia zinasema kwamba kiungo huyo aliyeng' ara kwenye michuano ya kombe la Chalenji iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana, Kenya, amesema yuko tayari kujiunga na Yanga ambao wamemudhihirishia kumsajili. Hata hivyo Singida United nayo imeonyesha nia ya kumsajili lakini yeye mwenyewe amedai timu itakayofikia dau ndio itakayomchukua, mbali na Fei Toto, Yanga inadaiwa kumuhitaji kiungo mwingine Mzanzibar, Mudathil Yahya na kipa wa Zanzibar Abubakar Mohamed Fesal Salum "Fei Toto" (Wa tatu kutoka kulia) anakwenda Yanga

AZAM FC KUIFUATA STAND UNITED NUSU FAINALI LEO?

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Mabingwa wa kombe la Mapinduzi, Azam Fc usiku wa leo wanashuka katika uwanja wao wa Azam Complex, Chamazi kuumana na Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani Morogoro mchezo wa robo fainali ya kombe la Azam Sports Feferation Cup. Jana Stand United imetangulia nusu fainali baada ya kuilaza Njombe Mji bao 1-0 katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, kwa maana hiyo mshindi kati ya Azam Fc na Mtibwa Sugar atakutana na Stand United kwenye nusu fainali. Mechi nyingine leo itapigwa uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine pale Mbeya wakati wenyeji Tanzania Prisons wakiwaalika wanajeshi wa JKT Tanzania mchezo wa robo fainali wa michuano hiyo, kesho pia kutakuwa na mchezo mwingine Yanga Sc wakiwa wageni wa Singida United uwanja wa Namfua mjini Singida Azam Fc inacheza na Mtibwa leo

Yanga yatua kibabe Singida, kummaliza Pluijm

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga Sc tayari kimewasili mjini Singida ambapo keshokutwa Jumapili siku ya Pasaka kitakwaruzana na wenyeji wao Singida United mchezo wa robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup, maarufu FA Cup. Yanga ilikuwa imeweka kambi Bigwa mjini Morogoro tangu majuzi ikitokea Dar es Salaam ikiwa na nyota wake wote isipokuwa wanne waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambao nao wakaungana na wenzao juzi. Hata hivyo huenda wachezaji wake wawili Maka Edward na Musa Mwinyi "Ronaldo" wakakosekana baada ya kuwepo kwenye na timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Heroes. Akizungumza jioni ya leo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Yanga, Dissmas Ten amesema kikosi kimetua salama Singida na kesho kitafanya mazoezi katika uwanja wa Namfua kabla ya keshokutwa kuumana na Singida United, hata hivyo Ten amedai wamejipanga kushinda mchezo Yanga wametua Singida leo

Stand United yawa ya kwanza kutinga nusu fainali FA Cup

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga imefanikiwa kuwa timu ya kwanza kutangulia kuingia nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup, baada ya kuilaza Njombe Mji ya Njombe bao 1-0. Mchezo huo wa robo fainali uliofanyika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, bao pekee la ushindi lilipatikana dakika ya 12 kipindi cha kwanza na Hamad Swahady aliyepokea pasi ya Vitalis Mayanga. Hata hivyo Stand United walimaliza mchezo wakiwa pungufu baada ya nahodha wake Alex Mulilo kuonyeshwa kadi mbili za manjano, kesho michuano hiyo itaendelea kati ya Tanzania Prisons na JKT Tanzania huku usiku Azam Fc itaialika Mtibwa Sugar Stand United imeingia nusu fainali

Simba yaiendea Njombe Mji, Iringa, kuwakosa Mkude, Bocco na Fabregas

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba Sc kesho Jumamosi wanatarajia kuelekea mkoani Iringa tayari kabisa kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu bara dhidi ya Mji Njombe Fc uwanja wa Sabasaba, Njombe Jumanne ya Aprili 3 mwaka huu. Vinara hao watakaa mjini Iringa hadi Jumatatu ambapo wataelekea Njombe, Simba itawakosa wachezaji wake wanne ambao ni majeruhi. Akizungumza na Mambo Uwanjani, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kikosi kitasafiri kesho kuelekea Iringa kabla ya kuifuata Njombe Mji, Jumatatu ambapo siku moja wataumana. Manara amesema Simba itamkosa kiungo wake Jonas Mkude ambaye aliumia kifundo cha mguu, pia itamkosa nahodha wake John Raphael Bocco ambaye aliumia, pia itaendelea kuwakosa Haruna Niyonzima na Salim Mbonde, Simba iko kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 46 na hiyo ni mechi ya kiporo Simba itaondoka kesho kuelekea Iringa

Abdulrahman Musa aibukia Mtambani

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting, jioni ya leo ameibukia katika timu ya Mtambani Fc ya Tabata jijini Dar es Salaam akiichezea kwenye michuano ya kuwania Ng' ombe mnyama iitwayo Tabata Super Cup. Katika mchezo uliofanyika uwanja wa Shule ya msingi Tabata, timu ya Mtambani Fc imeweza kuingia nusu fainali, baada ya kuilaza timu ya Amani City pia ya Tabata kwa mabao 2-0. Mtambani Fc walianza kusherehekea bao la kwanza lililofungwa kipindi cha kwanza na mshambuliaji Issa Pitchou kabla ya Abdulrahman Musa kufunga bao la pili la kichwa. Hadi mapumziko Mtambani ilikuwa mbele kwa mabao hayo mawili, kipindi cha pili hakikuwa na magoli zaidi ya Mtambani kucheza show game na kufurahisha mashabiki lukuki waliojazana uwanjani, Musa msimu huu amefunga goli moja tu kwenye Ligi Kuu inayoendelea hivyo inaonekana kama ameibukia Mtambani Abdulrahman Musa leo ameichezea Mtambani Fc 

ANAYEKUMBUKWA

Picha
ISSA ATHUMAN MGAYA: FUNDI WA MPIRA. Alianza kujulikana kama fundi seremala akitengeneza vitanda, makochi na meza kwa kutumia mbao, ujuzi huo alifundishwa na mjomba wake ambaye alizaliwa tumbo moja na mama yake mzazi. Hapa namzungumzia fundi wa mpira Issa Athuman Mgaya ambaye alicheza kwa mafanikio Yanga Sc na timu ya taifa, Taifa Stars miaka iliyopita. Nakumbuka wakati huo nilikuwa mdogo lakini nilikuwa mfutiliaji mkubwa wa mpira wa miguu, Issa alikuwa kiungo mkabaji wa Yanga mwenye uwezo wa kucheza sentahafu na aliweza kung' ara vilivyo kwenye kikosi hicho na kubahatika kwenda kucheza soka la kulipwa Uarabuni. Kwa miaka hiyo mchezaji wa Kitanzania ukisikia anaenda Uarabuni ujue huyo ni staa kwelikweli, basi Issa alibahatika kwenda Umangani, na aliporejea nchini alijiunga tena na Yanga. Nakumbuka kipindi hicho Yanga ilikuwa na nyota kama Steven Nemes, Seleman Mkati, Kenneth Mkapa, Godwin Aswile, Salum Kabunda, Abubakar Salum "Sure Boy" Justin Mtekele, Said Mwamba, Ed...

NIYONZIMA, BOCCO WAITISHA NJOMBE MJI

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc wanaendelea kujifua katika uwanja wa Boko Veteran mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji utakaofanyika Aprili 3 uwanja wa Saba Saba mjini Njombe. Vijana wa Njombe juzi walijinasibu kuwa hawaiogopi Simba na watatoa upinzani mkubwa kuhakikisha Simba haiondoki na pointi tatu, Lakini nyota watatu wa Simba ambao walikuwa majeruhi wamerejea uwanjani ambao ni straika John Bocco "Adebayor" ambaye ni nahodha, beki Salim Mbonde na kiungo hatari Haruna Niyonzima. Na kwa bahati nzuri Niyonzima aliyejiunga na Simba akitokea Yanga amesema huo utakuwa mchezo wake wa kwanza tangu kurejea kwake uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu na anataka kuwadhihirishia mashabiki wa Simba kuwa yeye ni nani. Niyonzima amedai mchezo huo atafanya kweli na kuweza kuing' arisha Simba kileleni, wakati Niyonzima akiyasema hayo, mshambuliaji John Bocco yeye ameda...

UREJEO WA NGOMA, TAMBWE NA KAMUSOKO WAIPASUA SINGIDA UNITED

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Hofu imetanda ndani ya kikosi cha Singida United hasa baada ya kurejea kwa nyota watatu wa mabingwa wa soka nchini Yanga Sc, Wazimbabwe, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Mrundi Amissi Tambwe ambao walikuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu. Nyota hao wapo kambini mjini Morogoro na kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyepo mazoezini anasema ni balaa tupu jamaa wapo vizuri kiasi kwamba kocha waabingwa hao Mzambia George Lwandamina roho kwatuu. Taarifa kutoka kwa Singida, zinadai kwa sasa timu ya Singida United imeingia mchecheto baada ya kusikia ujio wa nyota hao watatu ambao wataungana na nyota wengine walioiweka Yanga hapo ilipo. Kocha wa Singida United, Mholanzi Hans Van der Pluijm hajui nini kitatokea katika mchezo wao na Yanga utakaopigwa uwanja wa Namfua mjini Singida Aprili 1 mwaka huu kwani anakijua kikosi cha Yanga lakini Ngoma, Kamusoko na Tambwe wanamuumiza kichwa kwani bado Tshishimbi, Chirwa, Ajibu na Hassan Kessy wanamnyima usingizi Kurejea...

SAMATTA, KICHUYA WAING' ARISHA STARS

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo imefanikiwa kung' ara baada ya kuilaza timu ya taifa ya DR Congo, Leopards mabao 2-0 mchezo wa kirafiki wa kimataifa uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. DR Congo ikicheza na mastaa wake wanaocheza barani Ulaya walishindwa kutamba mbele ya Tanzania iliyokuwa na mchezaji mmoja tu anayecheza Ulaya, hadi mapumziko timu zote hazikufungana. Kipindi cha pili kilikuwa kizuri kwa Stars inayonolewa na Salum Mayanga ambapo iliweza kujipatia mabao hayo mawili yaliyofungwa na Mbwana Samatta aliyepokea pasi ya Shiza Kichuya na goli la pili lilifungwa na Shiza Kichuya aliyepokea pasi ya Mbwana Samatta. Kwa matokeo hayo Stars inaweza kukwea katika viwango vya Fifa kwani washindani wao DR Congo wanashikilia nafasi ya 39 duniani na 3 Afrika wakati Tanzania ni ya 146 duniani na 41 Afrika Taifa Stars imeisurubu DR Congo 2-0 leo

Taarifa za Mkude kuvunjika kifundo cha mguu hizi hapa

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kiungo mahiri na bora kwa sasa hapa nchini, Jonas Gerald Mkude jana amevunjika kifundo cha mguu akiwa katika mazoezi ya klabu yake ya Simba Sc  yaliyofanyika kwenye uwanja wa Boko Veteran. Taarifa ambazo Mambo Uwanjani imezinyaka, zinasema kuwa kiungo huyo aliumia kifundo cha mguu na kushindwa kuendelea na mazoezi na kupelekea kurudishwa nyumbani kwake ni baada ya kufanyiwa rafu na kiungo mwenzake Muzamir Yassin. Daktari wa Simba, Yassin Gembe alishindwa kumpa matibabu kiungo huyo ili arejee mazoezi na badala yake alimruhusu aondoke huku akishindwa kukanyaga kwa miguu yote miwili kwani alikuwa akichechemea, Simba inajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu bara dhidi ya Njombe Mji, Aprili 3 mwaka huu uwanja wa Sabasaba mjini Njombe hivyo kunatilia shaka uwepo wa Mkude katika mchezo huo. Licha ya kuumia Mkude, jana majeruhi wawili wa muda mrefu, Haruna Niyonzima na Salim Mbonde wameanza mazoezi na kuna uwezekano mkubwa wa kuanza katika mchezo huo, Sim...

Stars na DR Congo kuonyeshana undava leo Taifa

Picha
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo inashuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mechi ya kirafiki inayotambuliwa na Fifa dhidi ya Chui ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC. Stars inayonolewa na mzalendo Salum Mayanga itakuwa na kazi kubwa kusaka ushindi katika mchezo huo kwani katika mchezo uliopita wa ugenini dhidi ya Algeria ilichapwa mabao 4-1. Licha ya leo Stars kuwatumainia nyota wake wanaocheza soka la kulipwa ughaibuni, Mbwana Ally Samatta, Simon Msuva na Abdi Banda lakini inaweza isifue dafu mbele ya DRC yenye nyota kibao wanaocheza barani Ulaya na Asia Taifa Stars itaumana na Dr Congo leo

Simba na Yanga sasa Aprili 29

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Bodi ya Ligi imetangaza rasmi pambano la watani wa jadi Simba na Yanga kuchezwa Aprili 29 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema kuwa mabadiliko ya mechi hiyo yametokana na Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, CAF kuipangia Yanga mchezo dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia kwenye tarehe ambayo ingepigwa mechi hiyo ya watani. Awali Simba na Yanga ilikuwa ipigwe Aprili 7 mwaka huu lakini imesogezwa hadi Aprili 29, pia Wambura amesema Bodi ya Ligi haitapangua mchezo kati ya Simba na Njombe Mji uliopangwa kufanyika Aprili 3 mwaka huu mjini Njombe na amewataka Njombe kucheza mechi hiyo Simba na Yanga zitaumana Aprili 29 mwaka huu

Kispoti;

Picha
Mayanga kosa lake liko wapi! asihukumiwe Na Prince Hoza KELELE zimekuwa nyingi mno kutoka kwa wadau na mashabiki wa soka zikimsakama kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Shaaban Mayanga. Kelele hizo nyingine zikimtaka ajiweke kando kuinoa timu hiyo, yote yanakuja kufuatia timu hiyo ya taifa kuchapwa mabao 4-1 na Algeria mchezo wa kirafiki unaotambuliwa na Shirikisho la mpira wa miguu duniani (Fifa). Mchezo huo ulifanyika nchini Algeria, hivyo timu hiyo ilisafiri kutoka Dar es Salaam hadi mjini Algiers kuwafuata Mbweha hao wa Jangwani, Stars iliingia kambini mapema juma lililopita kujiandaa na mechi mbili za kirafiki za kimataifa. Mchezo mwingine wa kirafiki unachezwa leo katika uwanja wa Taifa dhidi ya DR Congo, hivyo baada ya kupoteza ugenini kwa mabao hayo 4-1 Watanzania wameona tatizo lipo kwa kocha Mayanga. Kumlaumu kocha huyo hasa kwa kufungwa na Algeria sidhani kama kuna weledi umetumika wa kutosha katika kuutathimini mchezo huo dhidi ya timu kubwa ya...

Yanga waiendea Moro, Singida United

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kikosi cha mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc leo kinatarajia kuelekea mkoani Morogoro kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na mchezo wake wa Robo fainali dhidi ya Singida United kombe la Azam Sports Federation Cup uwanja wa Namfua mjini Singida. Yanga watasafiri na wachezaji wake wote isipokuwa wale waliopo kwenye timu za taifa za Taifa Stars na Ngorongoro Heroes. Wachezaji ambao watakosekana kwenye msafara huo ni Ibrahim Ajibu, Hassan Kessy, Ramadhan Kabwili na Kevin Yondan, wengine ni Maka Edward na Said Musa "Ronaldo" ambao hao wapo na Ngorongoro Heroes. Yanga ikishamaliza mchezo wake na Singida United, Aprili 1, itarejea Dar es Salaam kujiwinda na mchezo wa kuelekea hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia utakaopigwa Aprili 7 mwaka huu uwanja wa Taifa Dar es Salaam Yanga wameiendea Singida United, Morogoro

DRC WAJA NA MASTAA WAO KUINYOOSHA STARS KESHO

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kikosi cha timu ya taifa ya Jumuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamewasili mapema leo kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki wa FIFA dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars utakaopigwa kesho uwanja wa Taifa Dar es Salaam. kikosi hicho kinachonolewa na kocha mzawa Jean- Fkorent Ikwange Ibenge, kimekuja na mastaa wake wote wanaotesa kwa sasa katika vilabu mbalimbali. Timu hiyo imetua na mchezaji ghali wa Afrika anayeng' ara kwa sasa Cedric Bakambu aliyenunuliwa na klabu ya Beijing Guoan ya China akitokea kwa Villarreal ya Hispania kwa pauni Milioni 64. pia imetua na nyota wa West Ham, Bolasie Yannick na Chancel Mbemba wa New Castle zote za England na nyota mwingine Masuaku Arther anayecheza pia Ulaya. Kulingana na ujio wa mastaa hao ambapo wengine wanacheza katika vilabu vikubwa barani Afrika kama TP Mazembe na Raja Casablanca, kwa hakika Taifa Stars ya mzalendo Salum Mayanga itakuwa na kazi ngumu hiyo kesho kuanzia saa 10:00 kwa kiingili...

HATIMAYE DONALD NGOMA FITI KUZIVAA SINGIDA, DICHA

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Daktari mkuu wa mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc, Edward Bavu amemwashia taa ya kijani mshambuliaji hatari wa mabingwa hao nchini, Mzimbabwe, Donald Ngoma kurejea uwanjani na kucheza dhidi ya Singida United Aprili 1 na Welayta Dicha Aprili 8 kwakuwa yuko fiti kwa asilimia 89. Ngoma alikuwa majeruhi kwa muda mrefu tangia mzunguko wa kwanza lakini ni habari njema kabisa kwa mabingwa hao wa bara ambao wana mtihani mzito kusonga mbele katika mechi zake za mashindano. Mbali na kurejea kwa Donald Ngoma ambaye anasifika kwa upachikaji mabao, Mrundi, Amissi Tambwe naye amerejea uwanjani hivyo sasa kunawafanya Wanayanga kutuliza mioyo yao kwani mastaa wao wote sasa wamerejea baada ya hivi karibuni Mzimbabwe Thabani Kamusoko kurejea Donald Ngoma fiti kuzivaa Singida United na Welayta Dicha

MANYIKA JR AREJEA KUITIBULIA YANGA

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Kipa namba moja wa Singida United, Peter Manyika Jr hatimaye amerejea uwanjani baada ya kukosekana kwa muda mrefu akiuguza majeraha yake. Taarifa zilizotolewa jana na uongozi wa Singida United zinasema kuwa kipa huyo huenda sasa akakaa langoni kuivaa Yanga katika mchezo wa kombe la Azam Sports Federation Cup hapo Aprili 1 hatua ya Robo fainali itakayopigwa uwanja wa Namfua mjini Singida. Manyika Jr amekuwa msaada mkubwa kwenye kikosi hicho na kurejea kwake kunaibua hofu kwa mabingwa wa soka nchini Yanga Sc ambao wanaijua vema shughuri ya mlinda mlango huyo ambaye ni mtoto wa kipa wao wa zamani, Manyika Peter Manyika Peter Manyika Jr amerejea tena langoni

DOGO JANJA AWEKWA MTEGONI NA MKEWE

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Hatimaye msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Dogo Janja amejikuta akiwekwa mtegoni na mke wake Irene Uwoya ambaye ni staa pia wa tasnia ya filamu nchini. Wawili hao walifunga ndoa yapata miezi mitano iliyopita na mpaka sasa ndoa yao imefikia patamu ambapo kila mmoja amekuwa akimwonea wivu mwenziye. Lakini kwa Dogo Janja mambo yamekuwa magumu hasa baada ya kuzuiwa na mkewe kujihusisha na wanawake wengine ikiwemo hata kuwashirikisha kwenye video yake ya wimbo mpya Wayu wayu. Katika video hiyo, Dogo Janja imemlazimu kushiriki kama mwanamke hasa baada ya kutakiwa asimshirikishe mwanamke mwingine, kuhusu upendo, Dogo Janja alipoulizwa na chombo kimoja cha habari alisema anampenda mkewe kwa asilimia 100 wakati Uwoya alipoulizwa naye akasema anampenda Janjaro kwa asilimia 80 Dogo Janja awekwa mtegoni na mkewe

KIUNGO YANGA ADAIWA KUTELEKEZA MTOTO, AFA

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Kiungo mshambuliaji wa klabu bingwa ya soka nchini, Yanga Sc, Geofrey Mwashiuya, inadaiwa ametelekeza mtoto na kwa bahati mbaya mtoto huyo amefariki dunia hivi karibuni baada ya kuungua na maji ya moto akiwa anacheza peke yake. Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya majirani, zinasema kuwa mtoto huyo mdogo alikuwa akicheza peke yake kwa bahati mbaya akamwagikiwa na maji ya moto yaliyokuwa jikoni na kumsababishia maumivu makali mwilini. Mtoto huyo inadaiwa kuwa ni wa mchezaji huyo wa Yanga lakini taarifa zinasema kuwa Mwashiuya alishamkataa baada ya kuzaliwa na hakuwahi kumuona, ila mzazi mwenzake anathibitisha kuwa ni wa Mwashiuya kwani alikuwa rafiki yake wa muda mrefu. Mtoa taarifa hizi anasema Mwashiuya alipigiwa simu kujulishwa kifo cha mwanaye lakini aliwajibu kuwa Yanga imemzuia kutoka kambini hivyo hawezi kuhudhuria mazishi. Mungu ailaze mahari pema peponi roho ya mtoto huyo asiye na hatia yoyote Geofrey Mwashiuya ametelekeza mtoto

Lwandamina aihofia Welayta Dicha

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kocha mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc, George Lwandamina raia wa Zambia amesema timu ya Welaiyta Dicha ya Ethiopia si timu ya kubeza na wala siyo njia nyepesi kwa Yanga kusonga mbele. Akizungumza kwa simu akitokea kwao Zambia ambapo yupo kwa mapumziko, amedai timu hiyo ya Ethiopia ambao ni mabingwa wa kombe la Ligi nchini humo ni moja kati ya timu ngumu na tishio. Amedai timu hiyo imeweza kuziondoa timu za Zimamoto ya Zanzibar na Zamalek ya Misri hivyo siyo ya kuibeza hata kidogo, Yanga imepangwa kucheza na Dicha kati ya Aprili 6 au 8  Dar es Salaam na kurudiana Aprili 17 au 18 Addis Ababa, Lwandamina amedai kujifua ndio njia nzuri kwao kufanya vizuri kuelekea mchezo huo Kocha wa Yanga, Mzambia George Lwandamina anaihofia Welayta Dicha

Njombe waapa kuivurugia Simba, lakini wagomea mchezo

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Uongozi na wachezaji wa timu ya Njombe Mji ya mkoani Njombe wamewaahidi mashabiki wao kwamba watapambana ili wasishuke daraja msimu huu pia hawatakubali kugeuzwa ngazi na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc watakapoumana Aprili 3 mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa uwanja wa Sabasaba mjini Njombe. Wakizungumza na Mambo Uwanjani, baadhi ya wachezaji wa Njombe Mji wamesema iwe isiwe hawatakubali kufungwa katika mechi zao zilizosalia ikiwemo dhidi ya Simba, wamesema mechi hiyo itawapa mzuka wa kufanya vema na kubakia Ligi Kuu. Hata hivyo taarifa zilizopatikana hivi punde zinasema Njombe Mji wameugomea mchezo huo kwa madai upo karibu na mchezo wao watakaocheza na Stand United wa kombe la FA, msemaji wa Njombe Mji, Hassan Mancho amedai haiwezekani wao kucheza ndani ya siku mbili. Wameitaka Bodi ya Ligi kuangalia vema kanuni kwani inaonekana wazi kuna njama za kutaka kuishusha daraja Njombe hasa kwa kuwapangia mechi tat...

WAMBURA AFUNGIWA MAISHA KUJIHUSISHA NA SOKA

Picha
Na Saida Salum. Dar es Salaam Kamati ya Maadili ilikutana tarehe 14/3/2018 kupitia shauri linalomhusu Ndugu Michael Richard Wambura, Makamu Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ambaye anashtakiwa na Sekretarieti ya TFF kwa makosa matatu ya kimaadili. *TUHUMA ZILIZOWASILISHWA * Sekretarieti ya TFF iliwasilisha mbele ya Kamati mashtaka matatu (3) ambayo ni; 1. /Kupokea/kuchukua fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo      hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha Kanuni za     Maadili za TFF Toleo la 2013./ 2. /Kughushi barua ya kuelekeza alipwe malipo ya kampuni ya JEKC     SYSTEMS LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume     na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013./ 3. /Kufanya vitendo vinavyoshusha Hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume     na ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (kama ilivyorekebishwa 2015)/ MAELEZO YA KOSA Ndugu Mi...

Tshishimbi awa mwanasoka bora Februali

Picha
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam Kiungo wa kimataifa wa mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc, Papy Kabamba Tshishimbi raia wa DR Congo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wa mwezi Februali. Kamati ya tuzo ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) kupitia Bodi ya Ligi, imeamua kumpa tuzo hiyo kiungo huyo mpambanaji uwanjani baada ya kuonekana ameisaidia timu yake ya Yanga kushinda mechi nne mfululizo huku akihusika kufunga mabao matatu. Tshishimbi amefanya vizuri zaidi katika mechi dhidi ya Majimaji, Njombe Mji, Ndanda Fc na Lipuli, kiungo huyo aliwabwaga Emmanuel Okwi wa Simba Sc na kiungo mshambuliaji, Pius Buswita pia wa Yanga, Tshishimbi atajinyakulia shilingi Milioni mbili pamoja na king' amuzi kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo Vodacom na Azam Tv Papy Kabamba Tshishimbi awa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara, Februali

Yanga yaifuata kibabe Township Rollers

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga Sc wameondoka alfajiri ya leo kuelekea Gabolone Botswana kwa ajili ya mchezo wake wa marudiano dhidi ya Township Rollers wiki hii. Mabingwa hao wanekwea pipa alfajiri ya saa 10:00 na nyota wake 20, Yanga inahitaji ushindi wa mabao 2-0 au zaidi ili kuingia hatua ya makundi ama sivyo itaondolewa mashindanoni. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Dar es Salaam juma lililopita, Yanga ilikubali kipigo cha mabao 2-1 na kujiweka katika mazingira magumu, lakini mabingwa hao wa Bara wameenda Botswana wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuichapa Stand United mabao 3-1 na kufanikiwa kuwakamata mahasimu wao kileleni Simba Sc wenye pointi 46 na sasa timu hizo zinazidiana mabao ya kufunga tu Yanga wameondoka leo kuelekea Botswana

Yanga yaikamata Simba kileleni

Picha
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga Sc jioni ya leo imefanikiwa kuilaza Stand United mabao 3-1 mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam. Yanga walijipatia mabao mawili mapema, moja likifungwa dakika ya sita na Yusuphu Mhiru na lingine likifungwa na Ibrahim Ajibu dakika ya 12, timu hizo zilienda kupumzika Yanga ikiwa mbele. Kipindi cha pili Stand United walilishambulia lango la Yanga wakitaka kusawazisha na wakafanikiwa kupata bao kupitia Vitalis Mayanga, kabla ya Obrey Chirwa kufunga bao la tatu. Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 46 sawa na mahasimu wao Simba Sc wanaoongoza ligi hiyo na sasa Yanga ni ya pili

Simba yatajwa na CAF klabu tajiri zaidi Afrika

Picha
Klabu ya  Simba ya Jijini Dar es Salaam imetajwa na shirikisho la soka Afrika (CAF) kuwa klabu namba 5 kwa utajiri Barani Afrika. Simba imetajwa kuwa na utajiri wa karibu Paund Milioni 10.35 ambayo ni sawa na Bilioni 32.3 kwa shilingi ya Tanzania. Katika orodha hiyo Al Ahly kutoka Misri inaongoza ikiwa na utajiri wa Paund Milioni 19.25 ikifuatiwa na Esperance Sportive de Tunis (12.75M)na Club Africain (11.8M) zote kutoka Tunisia. Ya nne ni Kaizer Chief ya kutoka nchini Afrika Kusini ambayo yenyewe inautajiri karibu Paund Milioni 10.48. Klabu tajiri zaidi barani Afrika.  1. Al Ahly(Egypt) - €19,25M. 2. Esperance Sportive de Tunis( Tunisia)- €12,75M. 3. Club Africain ( Tunisia)- 11,80M 4. Kaizer Chiefs( South Africa)-€ 10,48M 5. Simba Sports Club (Tanzania)- €10,35M 6. Zamalek SC (Egypt) - €10,30M. 7. USM Alger( Algeria)- Market € 9,65M. 8. ES Serif ( Algeria)-8,60M. 9. Raja Casablanca( Morocco)- €8,13M 10. TP Mazembe( DRC)- €7,70M Simba imetajwa na CAF moj...

YANGA KUIKAMATA SIMBA KILELENI LEO?

Picha
Na Prince Hoza. Dar es Salaam Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga Sc, huenda leo ikaikamata Simba Sc kileleni itakapotelemka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuikaribisha Stand United ya Shinyanga mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 43 lakini inaweza kuchupa hadi nafasi ya kwanza ama ya pili endapo itaibuka na ushindi dhidi ya Stand United kwani itafikisha pointi 46 ambazo zinamilikiwa pia na vinara wa ligi hiyo Simba Sc. Stand United siyo timu ya kubeza kwani imeweza kuitoa nishai Simba kwa kuilazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, hivyo na leo wanaweza kufanya maajabu kwa mabingwa hao watetezi ambao msimu huu wanaonekana kuchechemea Yanga wanaweza kuishika Simba kileleni leo