SAMATTA, KICHUYA WAING' ARISHA STARS
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo imefanikiwa kung' ara baada ya kuilaza timu ya taifa ya DR Congo, Leopards mabao 2-0 mchezo wa kirafiki wa kimataifa uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
DR Congo ikicheza na mastaa wake wanaocheza barani Ulaya walishindwa kutamba mbele ya Tanzania iliyokuwa na mchezaji mmoja tu anayecheza Ulaya, hadi mapumziko timu zote hazikufungana.
Kipindi cha pili kilikuwa kizuri kwa Stars inayonolewa na Salum Mayanga ambapo iliweza kujipatia mabao hayo mawili yaliyofungwa na Mbwana Samatta aliyepokea pasi ya Shiza Kichuya na goli la pili lilifungwa na Shiza Kichuya aliyepokea pasi ya Mbwana Samatta.
Kwa matokeo hayo Stars inaweza kukwea katika viwango vya Fifa kwani washindani wao DR Congo wanashikilia nafasi ya 39 duniani na 3 Afrika wakati Tanzania ni ya 146 duniani na 41 Afrika