MAAFANDE WA JKT TANZANIA YAWAPIGISHA KWATA PRISONS KWAO

Na Exipedito Mataruma. Mbeya

Timu ya JKT Tanzania inayonolewa na Bakari Shime "Mchawi mweusi", imefanikiwa kuichapa Tanzania Prisons mabao 2-0 uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mechi ikipigwa mchana.

JKT Tanzania iliyopanda Ligi Kuu bara imeweza kutinga nusu fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup maarufu FA Cup baada ya ushindi huo wa leo ambapo sasa itaumana na mshindi kati ya Yanga Sc na Singida United itakayopigwa kesho.

Mabao ya washindi yametiwa kimiani na Ally Ahmed dakika ya 13 kipindi cha kwanza na Hassan Matelema dakika ya 78 kipindi cha pili, mchezo mwingine wa robo fainali ya michuano hiyo itapigwa usiku wa leo kati ya Azam Fc na Mtibwa Sugar uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam

JKT Tanzania imeifunga Prisons 2-0

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA