Lwandamina aihofia Welayta Dicha
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Kocha mkuu wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga Sc, George Lwandamina raia wa Zambia amesema timu ya Welaiyta Dicha ya Ethiopia si timu ya kubeza na wala siyo njia nyepesi kwa Yanga kusonga mbele.
Akizungumza kwa simu akitokea kwao Zambia ambapo yupo kwa mapumziko, amedai timu hiyo ya Ethiopia ambao ni mabingwa wa kombe la Ligi nchini humo ni moja kati ya timu ngumu na tishio.
Amedai timu hiyo imeweza kuziondoa timu za Zimamoto ya Zanzibar na Zamalek ya Misri hivyo siyo ya kuibeza hata kidogo, Yanga imepangwa kucheza na Dicha kati ya Aprili 6 au 8 Dar es Salaam na kurudiana Aprili 17 au 18 Addis Ababa, Lwandamina amedai kujifua ndio njia nzuri kwao kufanya vizuri kuelekea mchezo huo