Tshishimbi awa mwanasoka bora Februali
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Kiungo wa kimataifa wa mabingwa wa soka nchini, Yanga Sc, Papy Kabamba Tshishimbi raia wa DR Congo amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wa mwezi Februali.
Kamati ya tuzo ya Shirikisho la mpira wa miguu nchini, (TFF) kupitia Bodi ya Ligi, imeamua kumpa tuzo hiyo kiungo huyo mpambanaji uwanjani baada ya kuonekana ameisaidia timu yake ya Yanga kushinda mechi nne mfululizo huku akihusika kufunga mabao matatu.
Tshishimbi amefanya vizuri zaidi katika mechi dhidi ya Majimaji, Njombe Mji, Ndanda Fc na Lipuli, kiungo huyo aliwabwaga Emmanuel Okwi wa Simba Sc na kiungo mshambuliaji, Pius Buswita pia wa Yanga, Tshishimbi atajinyakulia shilingi Milioni mbili pamoja na king' amuzi kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo Vodacom na Azam Tv