Abdulrahman Musa aibukia Mtambani
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita, Abdulrahman Musa wa Ruvu Shooting, jioni ya leo ameibukia katika timu ya Mtambani Fc ya Tabata jijini Dar es Salaam akiichezea kwenye michuano ya kuwania Ng' ombe mnyama iitwayo Tabata Super Cup.
Katika mchezo uliofanyika uwanja wa Shule ya msingi Tabata, timu ya Mtambani Fc imeweza kuingia nusu fainali, baada ya kuilaza timu ya Amani City pia ya Tabata kwa mabao 2-0.
Mtambani Fc walianza kusherehekea bao la kwanza lililofungwa kipindi cha kwanza na mshambuliaji Issa Pitchou kabla ya Abdulrahman Musa kufunga bao la pili la kichwa.
Hadi mapumziko Mtambani ilikuwa mbele kwa mabao hayo mawili, kipindi cha pili hakikuwa na magoli zaidi ya Mtambani kucheza show game na kufurahisha mashabiki lukuki waliojazana uwanjani, Musa msimu huu amefunga goli moja tu kwenye Ligi Kuu inayoendelea hivyo inaonekana kama ameibukia Mtambani