UREJEO WA NGOMA, TAMBWE NA KAMUSOKO WAIPASUA SINGIDA UNITED
Na Ikram Khamees. Dar es Salaam
Hofu imetanda ndani ya kikosi cha Singida United hasa baada ya kurejea kwa nyota watatu wa mabingwa wa soka nchini Yanga Sc, Wazimbabwe, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko na Mrundi Amissi Tambwe ambao walikuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.
Nyota hao wapo kambini mjini Morogoro na kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyepo mazoezini anasema ni balaa tupu jamaa wapo vizuri kiasi kwamba kocha waabingwa hao Mzambia George Lwandamina roho kwatuu.
Taarifa kutoka kwa Singida, zinadai kwa sasa timu ya Singida United imeingia mchecheto baada ya kusikia ujio wa nyota hao watatu ambao wataungana na nyota wengine walioiweka Yanga hapo ilipo.
Kocha wa Singida United, Mholanzi Hans Van der Pluijm hajui nini kitatokea katika mchezo wao na Yanga utakaopigwa uwanja wa Namfua mjini Singida Aprili 1 mwaka huu kwani anakijua kikosi cha Yanga lakini Ngoma, Kamusoko na Tambwe wanamuumiza kichwa kwani bado Tshishimbi, Chirwa, Ajibu na Hassan Kessy wanamnyima usingizi