Stars na DR Congo kuonyeshana undava leo Taifa
Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars jioni ya leo inashuka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kucheza mechi ya kirafiki inayotambuliwa na Fifa dhidi ya Chui ya jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
Stars inayonolewa na mzalendo Salum Mayanga itakuwa na kazi kubwa kusaka ushindi katika mchezo huo kwani katika mchezo uliopita wa ugenini dhidi ya Algeria ilichapwa mabao 4-1.
Licha ya leo Stars kuwatumainia nyota wake wanaocheza soka la kulipwa ughaibuni, Mbwana Ally Samatta, Simon Msuva na Abdi Banda lakini inaweza isifue dafu mbele ya DRC yenye nyota kibao wanaocheza barani Ulaya na Asia