YANGA KUIKAMATA SIMBA KILELENI LEO?
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Klabu bingwa ya soka Tanzania Bara, Yanga Sc, huenda leo ikaikamata Simba Sc kileleni itakapotelemka uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuikaribisha Stand United ya Shinyanga mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 43 lakini inaweza kuchupa hadi nafasi ya kwanza ama ya pili endapo itaibuka na ushindi dhidi ya Stand United kwani itafikisha pointi 46 ambazo zinamilikiwa pia na vinara wa ligi hiyo Simba Sc.
Stand United siyo timu ya kubeza kwani imeweza kuitoa nishai Simba kwa kuilazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 uwanja wa Taifa Dar es Salaam, hivyo na leo wanaweza kufanya maajabu kwa mabingwa hao watetezi ambao msimu huu wanaonekana kuchechemea