FEI TOTO ANAKWENDA YANGA
Na Prince Hoza. Dar es Salaam
Kiungo mahiri wa JKU na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes pamoja na Taifa Stars, Fesal Salum "Fei Toto" anakaribia kujiunga na mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga Sc iwapo itampa dau analotaka.
Taarifa zenye uhakika zilizotufikia zinasema kwamba kiungo huyo aliyeng' ara kwenye michuano ya kombe la Chalenji iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana, Kenya, amesema yuko tayari kujiunga na Yanga ambao wamemudhihirishia kumsajili.
Hata hivyo Singida United nayo imeonyesha nia ya kumsajili lakini yeye mwenyewe amedai timu itakayofikia dau ndio itakayomchukua, mbali na Fei Toto, Yanga inadaiwa kumuhitaji kiungo mwingine Mzanzibar, Mudathil Yahya na kipa wa Zanzibar Abubakar Mohamed