Yanga yatua kibabe Singida, kummaliza Pluijm

Na Mrisho Hassan. Dar es Salaam

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga Sc tayari kimewasili mjini Singida ambapo keshokutwa Jumapili siku ya Pasaka kitakwaruzana na wenyeji wao Singida United mchezo wa robo fainali ya kombe la Azam Sports Federation Cup, maarufu FA Cup.

Yanga ilikuwa imeweka kambi Bigwa mjini Morogoro tangu majuzi ikitokea Dar es Salaam ikiwa na nyota wake wote isipokuwa wanne waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambao nao wakaungana na wenzao juzi.

Hata hivyo huenda wachezaji wake wawili Maka Edward na Musa Mwinyi "Ronaldo" wakakosekana baada ya kuwepo kwenye na timu ya taifa ya vijana Ngorongoro Heroes.

Akizungumza jioni ya leo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Yanga, Dissmas Ten amesema kikosi kimetua salama Singida na kesho kitafanya mazoezi katika uwanja wa Namfua kabla ya keshokutwa kuumana na Singida United, hata hivyo Ten amedai wamejipanga kushinda mchezo

Yanga wametua Singida leo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA