Simba na Yanga sasa Aprili 29
Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam
Bodi ya Ligi imetangaza rasmi pambano la watani wa jadi Simba na Yanga kuchezwa Aprili 29 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema kuwa mabadiliko ya mechi hiyo yametokana na Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika, CAF kuipangia Yanga mchezo dhidi ya Welayta Dicha ya Ethiopia kwenye tarehe ambayo ingepigwa mechi hiyo ya watani.
Awali Simba na Yanga ilikuwa ipigwe Aprili 7 mwaka huu lakini imesogezwa hadi Aprili 29, pia Wambura amesema Bodi ya Ligi haitapangua mchezo kati ya Simba na Njombe Mji uliopangwa kufanyika Aprili 3 mwaka huu mjini Njombe na amewataka Njombe kucheza mechi hiyo