NIYONZIMA, BOCCO WAITISHA NJOMBE MJI
Na Saida Salum. Dar es Salaam
Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc wanaendelea kujifua katika uwanja wa Boko Veteran mjini Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji utakaofanyika Aprili 3 uwanja wa Saba Saba mjini Njombe.
Vijana wa Njombe juzi walijinasibu kuwa hawaiogopi Simba na watatoa upinzani mkubwa kuhakikisha Simba haiondoki na pointi tatu, Lakini nyota watatu wa Simba ambao walikuwa majeruhi wamerejea uwanjani ambao ni straika John Bocco "Adebayor" ambaye ni nahodha, beki Salim Mbonde na kiungo hatari Haruna Niyonzima.
Na kwa bahati nzuri Niyonzima aliyejiunga na Simba akitokea Yanga amesema huo utakuwa mchezo wake wa kwanza tangu kurejea kwake uwanjani baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu na anataka kuwadhihirishia mashabiki wa Simba kuwa yeye ni nani.
Niyonzima amedai mchezo huo atafanya kweli na kuweza kuing' arisha Simba kileleni, wakati Niyonzima akiyasema hayo, mshambuliaji John Bocco yeye amedai ataendelea kutupia mabao kuhakikisha Simba inakuwa bingwa msimu huu, kwa kauli hizo ni kama wanaitisha Njombe Mji ambao wapo katika janga la kushuka daraja