Njombe waapa kuivurugia Simba, lakini wagomea mchezo

Na Salum Fikiri Jr. Dar es Salaam

Uongozi na wachezaji wa timu ya Njombe Mji ya mkoani Njombe wamewaahidi mashabiki wao kwamba watapambana ili wasishuke daraja msimu huu pia hawatakubali kugeuzwa ngazi na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc watakapoumana Aprili 3 mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Wakizungumza na Mambo Uwanjani, baadhi ya wachezaji wa Njombe Mji wamesema iwe isiwe hawatakubali kufungwa katika mechi zao zilizosalia ikiwemo dhidi ya Simba, wamesema mechi hiyo itawapa mzuka wa kufanya vema na kubakia Ligi Kuu.

Hata hivyo taarifa zilizopatikana hivi punde zinasema Njombe Mji wameugomea mchezo huo kwa madai upo karibu na mchezo wao watakaocheza na Stand United wa kombe la FA, msemaji wa Njombe Mji, Hassan Mancho amedai haiwezekani wao kucheza ndani ya siku mbili.

Wameitaka Bodi ya Ligi kuangalia vema kanuni kwani inaonekana wazi kuna njama za kutaka kuishusha daraja Njombe hasa kwa kuwapangia mechi tatu mfululizo

Njombe Mji wameapa kuivurugia Simba

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA