DRC WAJA NA MASTAA WAO KUINYOOSHA STARS KESHO

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Kikosi cha timu ya taifa ya Jumuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wamewasili mapema leo kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki wa FIFA dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars utakaopigwa kesho uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

kikosi hicho kinachonolewa na kocha mzawa Jean- Fkorent Ikwange Ibenge, kimekuja na mastaa wake wote wanaotesa kwa sasa katika vilabu mbalimbali.

Timu hiyo imetua na mchezaji ghali wa Afrika anayeng' ara kwa sasa Cedric Bakambu aliyenunuliwa na klabu ya Beijing Guoan ya China akitokea kwa Villarreal ya Hispania kwa pauni Milioni 64.

pia imetua na nyota wa West Ham, Bolasie Yannick na Chancel Mbemba wa New Castle zote za England na nyota mwingine Masuaku Arther anayecheza pia Ulaya.

Kulingana na ujio wa mastaa hao ambapo wengine wanacheza katika vilabu vikubwa barani Afrika kama TP Mazembe na Raja Casablanca, kwa hakika Taifa Stars ya mzalendo Salum Mayanga itakuwa na kazi ngumu hiyo kesho kuanzia saa 10:00 kwa kiingilio cha shilingi 5000 mzunguko

DRC walipowasili leo kwa ajili ya kucheza na Tanzania kesho

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA